Druckschrift 
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
 

Kiongozi cha Sheria Imekuwa ni vigumu kwa watu wanaoishi vijijini kuthibitisha kuwa marehemu aliacha mila zake hali alikuwa akiishi kijijini na kushirikiana na wanakijiji katika shughuli mbalimbali za mila zao hata kama yeye mwenyewe haamini na hafuati. Swali Je Sheria za Kimila za Mirathi zinalingana na hali halisi ya maisha ya sasa? Toa maoni yako. Mifano ya Maamuzi ya Kesi Mahakimu na majaji wanasema kwamba, ikiwa sheria hii ya kimila inambagua mwanamke, wananchi wenyewe wanapaswa kupinga na kusema kwamba ni mbaya na haifai kwa kizazi hiki na kijacho. WANASISITIZA kuwa, sio mtu binafsi au kikundi cha watu wachache ndiyo wafanye hivyo bali jumuiya nzima iipinge sheria hii na wawasukume wabunge wao walifikishe suala hili bungeni ili sheria hii ibadilishwe.(Hii imenukuliwa kutoka kwenye Kesi ya Marko Kajubi dhidi ya Kualanima Kabali EACA 34-39. Katika kesi ya Bi Verdiana Kyabuje na wengine dhidi ya Gregory Kyabuje, Jaji Hamlyn alisema kwamba, ingawa Mahakama inakubaliana na upande wa mrufani kwamba kutofautisha wanawake na wanaume ni ubaguzi na inamnyanyasa mwanamke, Mahakama haina nguvu kupinga Sheria za Kimila. Mila hizi zinapaswa kubadilishwa na wananchi wenyewe. Kesi ya Felista Ishekanyoro dhidi ya Martin Banyika 1968 H.C.D. 112 pia inazungumzia mirathi. Maelezo: Felista alikuwa mke wa Banyika, Martin alikuwa mtoto wa Banyika kwa mke mwingine ambao walikuwa wameachana naye 89