Evans Robson Nzowa ni wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Alipata shahada ya kwanza ya Sheria mwaka 2000 kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Ndugu Nzowa kwa sasa ni Mwanasheria wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Mabenki, Huduma, Biashara na Kilimo [FIBUCA]. ISBN No. 9987- 22- 097- 5 Chapa na Ecoprint Ltd, Barua pepe: ecoprint@bol.co.tz Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi Tanzania Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi- Tanzania (A Simplified Version of the Tanzania Labour Law) Sheria ya Majadiliano ya Utumishi wa Umma Na. 19 ya 2003 Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya 2004 Sheria ya Asasi za Kazi Na. 7 ya 2004 kÎ?à?ŠŇ Þ žMŞšÌ!äžÞ? Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi- Tanzania Sheria ya Majadiliano ya Utumishi wa Umma Na. 19 ya 2003 Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya 2004 Sheria ya Asasi za Kazi Na. 7 ya 2004 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Kimepigwa Chapa na: ECOPRINT LTD, S.L.P 65182, Dar es Salaam, Simu: 022 2863864, 2865738 Barua pepe: ecoprint@bol.co.tz ISBN 9987- 22- 096-7 © Kitabu hiki hakiruhusiwi kunakilishwa au kupigwa chapa bila idhini ya Friedrich Ebert Stiftung S.L.P 4472 Dar es Salaam, Simu:+255 22 2668575/ 2668786 Fax:+255 22 2668669 ii Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania YALIYOMO UKURASA I Utangulizi......................................................................................... 1 1. Wafanyakazi wanaohusika na Sheria.......................................... 1 2. Madhumuni ya Sheria................................................................. 1 II Asasi za Kazi.................................................................................... 2 1. Baraza......................................................................................... 2 2. Tume........................................................................................... 3 3. Kamati........................................................................................ 3 4. Bodi............................................................................................. 4 5. Idara ya kazi............................................................................... 5 6. Mahakama ya Kazi..................................................................... 5 III Kinga za Msingi............................................................................... 6 1. Ajira ya mtoto............................................................................ 6 2. Ajira ya Shuruti.......................................................................... 6 3. Ubaguzi....................................................................................... 7 IV Viwango vya Ajira 1. Aina za Mikataba …………….........……………………...………. 9 2. Saa za kazi…………………………..........………………....……… 10 3. Ujira ……………....……………………..........…………………….. 15 4. Likizo …………………………………….........………….....……… 17 V Usitishaji Ajira ……………………………………………….........…… 21 1. Usitishaji ajira usio halali ……………………………...............…. 21 2. Usitishaji ajira kwa uonevu ………………………….........…....… 22 3. Usitishaji ajira kwa sababu ya utovu wa nidhamu …..........…… 22 4. Usitishaji ajira kwa sababu ya uwezo mdogo wa kazi…............. 25 5. Usitishaji ajira kwa sababu ya kutohitajika ………............…….. 29 6. Usitishaji ajira kwa sababu ya mahitaji ya uendeshaji …............ 30 iii Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania VI Uhuru wa Kujumuika na Vyama vya Wafanyakazi.......................... 35 1. Utaratibu wa kuunda Chama cha Wafanyakazi ………..........…. 36 2. Utaratibu wa kusajili Chama ……………………..............……… 36 3. Wajibu wa Chama kilichosajiliwa …………………..............…… 37 4. Wajibu wa kuzingatia Katiba ya Chama ………….....….........…. 38 5. Haki za Chama …………………………………......……..........…. 38 6. Haki ya kuingia eneo la Mwajiri ………....………..........……….. 38 7. Makato ya Ada …………………………….......……..........……… 39 8. Wawakilishi wa Chama………………......…………..........……… 39 9. Likizo……………………………........………………..........……… 40 10. Utaratibu wa kupata haki za Chama …………....….........……… 41 11. Usitishaji wa haki za Chama ……………….....……..........……… 41 VII Majadiliano ya pamoja…………..……………………..........………… 42 1. Utambuzi ….....……………………………………..........…………. 42 2. Utratibu wa Chama kuomba kutambuliwa ………........……….. 42 3. Jukumu la kujadiliana kwa nia njema ………………..........…….. 43 4. Masuala yanayoweza kujadiliwa katika majadiliano ya pamoja.................................................................................. 45 5. Jukumu la kutoa taarifa muhimu ……..……………….........…… 46 6. Utaratibu wa kuomba taarifa...……………….........……………. 46 7. Makubaliano ya pamoja …………………………..........………… 47 8. Makubaliano ya ada ya Uwakala …………………….........……. 47 9. Ushirikishwaji Wafanyakazi ………..….........……………………. 48 10. Kuondolewa kwa utambuzi …….…………..........……………….. 48 11. Utaratibu wa kuondoa utambuzi…….…………..........………….. 48 VIII Migomo ……………………………………………………........……... 49 1. Haki ya kugoma ………….……………………………..........…… 49 2. Kizuizi cha kugoma ………………………………………..........… 49 3. Utaratibu wa Mgomo……………………………….…...........…… 50 4. Vitendo vinavyokatazwa wakati wa mgomo…..………............… 50 5. Kiwango cha chini cha utoaji huduma …………………...........… 51 iv Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 6. Madhara ya mgomo usiofuata utaratibu au kutenda vitendo vinayokatazwa……………..…………..........….. 51 7. Kitendo cha kupinga ……………………………….............……… 51 8. Utaratibu wa kushiriki kitendo cha kupinga…………..........…… 51 9. Kizuizi cha kushiriki kitendo cha kupinga…………...........…….. 52 IX. Utatuzi wa Migogoro …………………………………..........………… 53 1. Mgogoro wa maslahi …………………………............…………… 53 2. Lalamiko …………………………………………..........………….. 53 3. Taratibu za utatuzi wa migogoro ya kazi …………..........……… 54 4. Usuluhishi …………………………………………...........………… 55 5. Uamuzi ……………………………………………............………… 56 6. Mahakama ……………………………………….............………… 58 7. Utatuzi wa migogoro kwa makubaliano…………............………. 60 X. Mabaraza ya Majadiliano ya Watumishi wa Umma.............………. 61 1. Uanzishwaji wa Mabaraza ya pamoja ………….........…......…… 61 2. Kazi za baraza la pamoja …………………............…...…………. 62 3. Maamuzi ya mabaraza ya pamoja ……………..........….....…….. 63 4. baraza kuu la pamoja la utumishi wa Umma ……..............……. 63 5. Kazi za baraza kuu la pamoja la utumishi wa umma...........….... 64 6. Kima cha chini cha mshahara ……………….................………… 64 7. Utaratibu wa kutoa ushauri na utatuzi wa migogoro ….............. 65 8. Makubaliano ……………………….......…………..........………… 66 9. Uwasilishaji mgogoro Mahakamani ……….....…..........………… 67 10. Utoaji Tuzo …………………………...................…………………. 67 11. Mgomo na kufungia nje …………….......….........……………….. 68 12. Baraza Kuu la Wafanyakazi …………..................………………. 69 XI. Viambatisho.............…….............................................................…. 73 1. Ajira na Mahusiano ya kazi........................................................ 91 2. Asasi............................................................................................ 175 v Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania DIBAJI Shirika lisilo la Kiserikali la Friedrich Ebert limekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Vyama vya Wafanyakazi duniani kote katika nyanja za maendeleo hususan uelimishaji. Kwa hapa Tanzania mahusiano hayo ya karibu yamekuwa kwa Vyama vya Wafanyakazi, pamoja na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania- TUCTA. Katika kitabu kilichotangulia cha“Mtaala ya Elimu kwa Vyama vya Wafanyakazi, kulikuwa na sura ya Sheria za Kazi. Sheria hizi ambazo ni mpya inabidi zieleweke katika matumizi yake. Hivyo basi baada ya kuutumia mtaala huo, wadau ambao ni wanachama wa Vyama vya Wafanyakazi walipendekeza kuwa Sheria hizo zitafsiriwe katika namna ambayo itawezesha matumizi yake kuwa rahisi. Kazi hii ambayo imechukua muda wa miezi tisa imetokana na mashauriano, na majaribio katika warsha mbalimbali. Ni mategemeo yetu kwamba mchango huu utasaidia kukikidhi kiu ya elimu kwa ajili ya wanachama wa Vyama vya Wafanyakazi- Tanzania na wale wote wenye kuhitaji kuelewa Sheria hizi za Kazi zinavyotumika au zinavyoweza kutumika. Nawatakia matumizi mema. Peter Haeussler Mkurugenzi Mkazi Friedrich Ebert Foundation December, 2009 vi Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania SURA YA KWANZA UTANGULIZI Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini ya mwaka 2004, iliyoanza kutumika tarehe 05/01/2007 ni matokeo ya mabadiliko ya sheria za kazi, yaliyotokana na sababu mbalimbali; ikiwa ni pamoja na:(a) Mabadiliko ya mfumo wa uchumi(uchumi wa soko) (b) Utandawazi (c) Mabadiliko ya siasa kutoka Chama kimoja kwenda vyama vingi vya siasa (d) Haja ya kuwa na vyama huru vya wafanyakazi (e) Kuzingatiwa kwa mapatano ya ILO (f) Mapungufu ya sheria zilizokuwepo Wafanyakazi wanaohusika na Sheria hii Sheria hii inawahusu wafanyakazi wote walioajiriwa Tanzania Bara isipokuwa walioajiriwa katika utumishi wa:(a) Jeshi la Wananchi wa Tanzania (b) Polisi (c) Magereza (d) Jeshi la Kujenga Taifa Madhumuni ya Sheria Madhumuni ya Sheria ni: (a) Kukuza uchumi kwa kuongeza ufanisi, tija na haki ya jamii. (b) Kuwa na mfumo wa sheria utakaohakikisha kuwapo uhusiano wenye ufanisi na wa haki katika ajira. Pamoja na kuweka viwango vya chini vya masharti ya kazi. (c) Kuwa na mfumo wa sheria utakaowezesha kufanyika majadiliano ya pamoja baina ya vyama vya Wafanyakazi na Waajiri au Jumuiya za Waajiri. (d) Kuthibiti matumizi ya mgomo na kufungia nje kama njia ya utatuzi wa migogoro ya kazi. (e) Kuwa na mfumo wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi, uamuzi na mahakama. (f) Kuingiza haki za kikatiba zinazohusiana na ajira katika sheria. (g) Kuzingatia mapatano ya ILO kwa kuyaingiza katika sheria. 1 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania SURA YA PILI ASASI ZA KAZI Asasi za kazi zimeanzishwa kwa mujibu wa Sheria za Asasi za Kazi, 2004 kila moja ikiwa na majukumu yake ya ushauri, usimamizi, kuzuia na kutatua migogoro ya kazi. Asasi hizo ni:(a) Baraza la kazi, uchumi na jamii(BARAZA) (b) Tume ya Usuluhishi na Uamuzi(TUME) (c) Kamati ya Huduma Muhimu(KAMATI) (d) Bodi za Ujira(BODI) (e) Usimamizi wa kazi na Ukaguzi(IDARA YA KAZI) (f) Mahakama ya kazi BARAZA Muundo wa Baraza Baraza linaundwa na Wajumbe 17, Mwenyekiti, Wajumbe wanne wanaowakilisha Wafanyakazi, Wajumbe wanne wanaowakilisha Waajiri, Wajumbe wanne wanaowakilisha Serikali na Wataalam wanne, wawili upande wa Wafanyakazi na wawili upande wa Waajiri. Kazi za Baraza Kazi za Baraza ni kuishauri Serikali kuhusu masuala yote yanayohusu Kazi, Uchumi na Jamii kama vile ukuzaji uchumi Sera za Soko la Ajira, mabadiliko ya Sheria za kazi n.k. Muda wa Wajumbe kukaa madarakani Wajumbe watakaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu na wanaweza kuteuliwa tena. 2 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania TUME Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ni Idara huru ya Serikali, ambayo kazi yake ni kusuluhisha na kuamua migogoro ya kazi. Tume pia inaweza kutoa ushauri na mafunzo kuhusu mbinu za kuzuia na kutatua migogoro, kusimamia uchaguzi wa Vyama vya Wafanyakazi na Jumuiya za Waajiri n.k. Mamlaka ya Wasuluhishi na Waamuzi Wasuluhishi na Waamuzi wana mamlaka ya:(a) Kumwita shaurini mtu yeyote kwa ajili ya kumuhoji au kuhudhuria shauri iwapo itaona mtu huyo ni muhimu katika kutatua mgogoro. (b) Kumwita mtu yeyote anayehodhi nyaraka au kitu chochote kinachohusika katika utatuzi wa mgogoro ili ahojiwe kuhusu nyaraka au kitu hicho au akiwasilishe mbele ya Tume (c) Kuapisha, kupokea uthibitisho kutoka kwa mashahidi. (d) Kumuhoji mtu yeyote kuhusu jambo lolote linalohusiana na mgogoro. KAMATI Kamati ya Huduma Muhimu ni sehemu ya Tume, na inaundwa na wajumbe watano wenye elimu, maarifa na uzoefu wa Sheria za Kazi na uhusiano kazini. Kazi za kamati ni:(a) Kubainisha na kutaja huduma muhimu kwa mujibu wa Sheria (b) Kuamua migogoro inayohusiana na huduma muhimu Kamati ina mamlaka ya:(a) Kumuita shaurini mtu yeyote kwa ajili ya kumuhoji, iwapo kuhudhuria kwake ni muhimu kuisaidia Kamati kutekeleza majukumu yake. (b) Kumuita mtu yeyote anayehodhi nyaraka au kitu chochote kinachohusiana na kazi za Kamati ili ahojiwe kuhusu nyaraka au kitu hicho au akiwasilishe mbele ya K amati. (c) Kuapisha, kupokea uthibitisho kutoka kwa mashahidi. (d) Kumuhoji mtu yeyote kuhusu jambo lolote linalohusiana na kazi za K amati. 3 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania BODI Bodi ya ujira zinaweza kuteuliwa kwa kuzingatia sekta au eneo. Bodi za ujira zinateuliwa na Waziri. Bodi za ujira zinaundwa na Wajumbe nane kwa kuzingatia utatu. Kazi za Bodi ni:(a) Kufanya uchunguzi kuhusu kima cha chini cha mshahara na masharti ya ajira (b) Kusaidia kuanzisha na kukuza majadiliano ya pamoja baina ya Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri (c) Kutoa mapendekezo kwa Waziri kuhusu kima cha chini cha mshahara na masharti ya ajira. Mamlaka (a) (b) (c) (d) ya Bodi Kumhoji mtu ambaye anaweza kutoa taarifa kuhusiana na uchunguzi inaoufanya Kumtaka mtu yeyote kwa maandishi kutoa taarifa, nyaraka, kitabu au kitu chochote kitakachosaidia uchunguzi Kuitisha mikutano ya hadhara Kuwezesha majadiliano ya pamoja kuhusu kima cha chini cha mshahara baina ya Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri au Jumuiya za Waajiri. Taarifa ya Bodi Bodi ikishamaliza uchunguzi wake itatoa taarifa yake kwa Waziri ikionyesha (a) Ung'amuzi wa Bodi (b) Mapendekezo kuhusu (i) Kima cha chini cha mshahara katika sekta au eneo husika (ii) Masharti yoyote maalum ya ajira katika sekta au eneo husika. Agizo au Tamko la Ujira Agizo au Tamko la ujira likitolewa na Waziri linabana Waajiri na Wafanyakazi katika sekta au eneo husika kuzingatia na linakuwa sehemu ya viwango vya ajira. 4 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania IDARA YA KAZI Idara ya Kazi inaongozwa na Kamishna wa Kazi na Naibu wake ambao uteuzi wao unafanywa na Rais, wakiwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria za Kazi. Chini yao wapo Makamishna wa Kazi wasaidizi watatu wanaoongoza Idara ya Uhusiano Kazini, Ukaguzi wa Kazi na Hifadhi ya Jamii. Na mwisho ni Maafisa wa Kazi. Mamlaka ya Maafisa wa Kazi Maafisa wa kazi wanayo mamlaka ya kuingia eneo la mwajiri kufanya ukaguzi, upekuzi, kukamata nyaraka, kuchukua sampuli, vipimo, kupiga picha, kumhoji mtu yeyote, kufungua mashitaka Mahakamani dhidi ya mtu anayekiuka Sheria za Kazi na kuendesha mashitaka kwa jina la Kamishna. Amri ya Kuzingatia Sheria Afisa wa Kazi anaweza kutoa amri ya kumtaka mwajiri azingatie Sheria za Kazi endapo atabaini mwajiri anakiuka Sheria za Kazi. MAHAKAMA YA KAZI Mahakama ya Kazi ni Divisheni ya Mahakama Kuu ya Tanzania. Mahakama itakuwa imetimia kwa ajili ya kusikiliza shauri iwapo Jaji atakuwa amekaa na waungwana washauri wa Mahakama wawili. Hata hivyo Jaji atakaa peke yake wakati wa:(a) Kusikiliza maombi (b) Wadaawa wakiamua washauri wasiwepo (c) Iwapo ni muhimu kwa utatuzi wa haraka wa mgogoro Uwakilishi Wadaawa wanaweza kuwakilishwa mbele ya Mahakama na:(a) Ofisa wa Chama cha Wafanyakazi, Jumuiya ya Waajiri; au (b) Wakili; au (c) Mtu yeyote wa chaguo lao Rufaa Rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Kazi zitapelekwa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwa masuala ya kisheria tu. 5 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania SURA YA TATU KINGA ZA MSINGI Sheria imeweka kinga maalum za msingi ili kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa ya staha na heshima kwa kukataza ajira ya mtoto, ajira ya shuruti na kupiga marufuku ubaguzi katika ajira. Makatazo haya yanawahusu pia, Jeshi la Wananachi wa Tanzania, Polisi, Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa. Katazo la ajira ya mtoto Ni marufuku kuajiri mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi na nne. Mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi, ambazo hazihatarishi au kuathiri afya yake, makuzi yake, mahudhurio shuleni au katika mafunzo, maadili n.k. Hairuhusiwi kumuajiri mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi na nane kufanya kazi katika migodi, viwanda na kwenye reli. Hata hivyo mtoto huyo anaweza kufanya kazi katika sehemu hizo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo chini ya usimamizi maalum. Katazo la ajira ya shuruti Hairuhusiwi kumshurutisha, au kumlazimisha mtu kufanya kazi pasipo ridhaa yake. Kazi za shuruti zinajumuisha pia kazi ambazo mtu hulazimika kufanya kulipia deni, kufanya akiwa amefungiwa au anazolazimika kuzifanya baada ya kupewa vitisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na kitisho cha kuadhibiwa. Hata hivyo kazi zifuatazo sio kazi za shuruti: (a) Kazi za kijeshi kwa mujibu wa sheria ya ulinzi wa taifa (b) Majukumu ya kawaida ya raia (c) Kazi katika kutekeleza hukumu au amri ya mahakama chini ya usimamizi wa mamlaka za serikali. (d) Kazi wakati wa hali ya hatari au majanga. (e) Kazi za jamii ambazo jamii yenyewe wamekubaliana kidemokrasia kuzifanya. 6 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Katazo la ubaguzi Waajiri wanakatazwa kuwabagua wafanyakazi wao kwa namna yoyote ile kwa misingi ya rangi, utaifa, kabila au sehemu ya asili atokapo mtu, mbali, utaifa wa asili, daraja la mtu katika jamii, itikadi ya siasa au imani ya kidini, jinsi, jinsia, ujauzito, hadhi ya ndoa au majukumu ya kifamilia, umri na ukimwi. Unyanyasaji ni ubaguzi pia. Hata hivyo sio ubaguzi:(a) Kutoa upendeleo maalum kwa madhumuni ya kuleta usawa na kuondoa ubaguzi mahali pa kazi. (b) Kumtofautisha, kumuondoa au kumpendelea mtu kutokana na mahitaji ya kazi. (c) Kuajiri raia kwa mujibu wa sheria. Waajiri ni lazima watengeneze mpango maalum unaoonyesha namna wanavyotoa fursa sawa na kuondoa ubaguzi mahali pa kazi na kuusajili mpango huo kwa Kamishna wa Kazi. Ni marufuku kwa vyama vya wafanyakazi, Jumuiya za Waajiri kufanya ubaguzi katika:(a) Kuingiza wanachama, kuwakilisha wanachama na kusitisha uanachama; (b) Sera na mazoea ya ajira; (c) Makubaliano ya pamoja. 7 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania SURA YA NNE VIWANGO VYA AJIRA. Viwango vya ajira ni masharti ya msingi katika ajira ambayo kila mwajiri anapaswa kuzingatia. Madhumuni ya kuwekwa viwango vya ajira ni kuwalinda wafanyakazi wasiingie katika mikataba ya ajira isiyo ya haki. Viwango hivi vinaweza kuboreshwa kupitia mkataba binafsi au makubaliano ya pamoja. Mkataba wa Ajira Msingi wa uhusiano wa kiajira baina ya mfanyakazi na mwajiri ni mkataba wa ajira. Mkataba wa ajira unaweza kuwa wa mdomo au wa maandishi. Ili kuhakikisha mambo ya msingi yanawekwa wazi Sheria inamtaka mwajiri kumpa mfanyakazi maelezo ya ajira yake kwa maandishi baada ya siku sita kuanzia siku ambayo mfanyakazi aliajiriwa, isipokuwa pale ambapo mfanyakazi amepewa mkataba wa maandishi ukiainisha waziwazi mambo hayo. Maelezo hayo ni haya yafuatayo: a) Jina, umri, anuani na jinsi ya mfanyakazi. b) Mahali pa kuajiriwa. c) Kazi za kufanya d) Tarehe ya kuanza kazi e) Aina ya muda wa mkataba f) Mahali pa kazi g) Saa za Kazi h) Ujira na marupurupu. Maelezo haya ni lazima yaeleweke vizuri kwa mfanyakazi. Mabadiliko yoyote ya maelezo ya ajira ni lazima yafanyike baada ya mwajiri kushauriana na mfanyakazi na kumpa taarifa ya mabadiliko hayo kwa maandishi. Maelezo haya ni lazima yaeleweke vizuri kwa mfanyakazi. Mabadiliko yoyote ya maelezo ya ajira ni lazima yafanyike baada ya mwajiri kushauriana na mfanyakazi na kumpa taarifa ya mabadiliko hayo kwa maandishi. 8 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Aina za Mikataba ya Ajira Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini imeigawa mikataba ya ajira katika aina kuu tatu: Mikataba isiyokuwa na Muda Maalum, Mikataba ya Muda Maalum na Mikataba ya Kazi Maalum. N Mikataba Isiyokuwa na Muda Maalum Mkataba usiokuwa na muda maalum ni mkataba ambao ukomo wa ajira haujatajwa waziwazi. Chini ya mkataba huu mfanyakazi anweza kuendelea na kazi mpaka kufikia umri wa kustaafu endapo haitatokea sababu yoyote ya kusitisha ajira kabla ya umri huo wa kustaafu. N Mkataba wa Muda Maalum Mkataba wa Muda Maalum ni mkataba ambao kipindi cha ajira kimewekwa wazi na tarehe ya ukomo wa ajira ipo wazi na inajulikana. Hata hivyo Sheria imeeleza wazi kuwa aina hii ya mkataba itawahusu waledi na wafanyakazi wa kada ya uongozi. N Mkataba wa Kazi Maalum Mkataba wa Kazi Maalum ni aina nyingine ya mkataba wa muda maalum ambao muda wake hutegemea kumalizika kwa kazi na malipo hufanyika kwa siku au baada ya kumalizika kwa kazi husika. N Wafanyakazi wasio na Mikataba inayoeleweka Waajiri wengi katika kukwepa haki za Kisheria za Wafanyakazi, huwafanyisha kazi wafanyakazi katika mtindo ambao uhusiano wa kiajira hauwekwi wazi. Kwa kuzingatia hali hiyo Sheria imeweka dhana inayokanushika na kuainisha vigezo ambavyo vikiwepo itachukuliwa kuwa uhusiano baina ya watu hao, anayefanya kazi na anayefanyiwa kazi ni uhusiano wa kiajira. Vigezo hivyo ni: N Namna ya ufanyaji kazi wa mtu huyo unasimamiwa na ni kwa maelekezo ya mtu mwingine. N Saa za kazi za mtu huyo zinasimamiwa na ni kwa maelekezo ya mtu mwingine. N Kwa mtu anayefanya kazi katika Shirika, mtu huyo ni sehemu ya Shirika. 9 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania N Mtu huyo amefanya kazi kwa mtu mwingine kwa wastani wa angalau saa 45 kwa mwezi katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. N Mtu huyo anamtegemea kiuchumi mtu anayemfanyia kazi au kumtolea huduma. N Mtu huyo anapatiwa vitendea kazi na mtu mwingine. N Mtu huyo anafanya kazi au kutoa huduma kwa mtu mmoja tu. Kuwepo kwa vigezo hivyo kunamaanisha kwamba mfanyakazi anachukuliwa kuwa ni mwajiriwa mpaka hapo itakapothibitika vinginevyo. SAA ZA KAZI Matumizi Wafanyakazi wanaosimamia na kuongoza wafanyakazi wengine kwa niaba ya mwajiri au mfanyakazi ambaye anaripoti moja kwa moja kwa kiongozi mwandamizi hawahusiki na kiwango cha saa za kazi. Saa za kazi za kawaida Saa za kazi za kawaida kwa mfanyakazi kufanya kazi ni saa 9 kwa siku na saa 45 kwa wiki. Siku za Kawaida za Kazi Siku za kawaida za kazi ni sita. Kwa kuzingatia ukomo wa saa 45 kwa wiki, ni dhahiri kuwa iwapo mfanyakazi anafanya kazi saa 9 kwa siku atafanya kazi siku 5 katika wiki na yule anayefanya kazi saa 8 kwa siku ndiye atafanya kazi siku 6 kwa wiki. Hata hivyo mfanyakazi anayefanya kazi saa 9 kwa siku anaweza kufanya kazi siku ya sita ambayo itakuwa ni saa za ziada. Saa za Ziada Kazi katika saa za ziada zitafanyika kwa makubaliano. Kwa msingi huo ili mfanyakazi afanye kazi saa za ziada ni lazima yawepo makubaliano, na makubaliano hayo yahakikishe saa za ziada hazizidi tatu(3) kwa siku na saa 50 katika mzunguko wa wiki. 10 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Mfanyakazi atakayefanya kazi saa za ziada anastahili kulipwa 1.5 ya mshahara wake wa saa kwa kila saa ya ziada aliyofanya kazi. Mfano Mshahara wa James ni sh. 150,000/= kwa mwezi. James amefanya saa za ziada 30 katika mwezi. Je! James atapata shilingi ngapi katika mwezi huo? Atapata 1: Mshahara wa saa: = 150,000 4.333 x 45 = 150,000 195 = 769/20 2: Saa za Ziada: = 769.20 x 1.5 x 30= 34,614 James atapata Tsh. 150,000/=+ 34,614/== 184,614/= Kazi za Sikukuu Mfanyakazi atakayefanya kazi siku za sikukuuu anastahili kulipwa mara mbili ya mshahara wake saa kwa kila saa aliyofanya kazi siku ya sikukuu. Mfano: Je! Endapo James alifanya pia saa 8 siku ya Sikukuu katika mwezi huo atalipwa sh. Ngapi? 769.20 x 2 x 8= 12,307.20 11 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Katika mwezi huo James atapata: = Mshahara = Saa za Ziada = Saa za Siku ya Sikukuu JUMLA 150,000/= 34,614/= 12,307.20 196,921.20/= Wiki ya kazi nyingi: Kwa makubaliano maalum, mfanyakazi anaweza kufanya kazi kwa saa 12 kwa siku bila kulipwa malipo ya saa za ziada, ili mradi mfanyakazi huyo asifanye kazi kwa zaidi ya saa 45 kwa wiki na si zaidi ya siku 5 kwa wiki na si zaidi ya saa za ziada 10 kwa wiki. Mfano Mfanyakazi anaweza kufanya kazi kwa utaratibu ufuatao katika wiki. = Jumatatu Saa 12 = Jumanne Saa 12 = Jumatano Saa 12 = Alhamisi Saa 9 JUMLA Saa 45 Endapo watafanya kazi na saa za ziada basi itabidi wafanye kazi kwa utaratibu ufuatao: = Jumatatu Saa 12 = Jumanne Saa 12 = Jumatano Saa 12 = Alhamisi Saa 12 = Ijumaa Saa 7 JUMLA Saa 55 * Alhamisi kuna saa 3 za ziada na Ijumaa saa zote 7 ni za ziada. 12 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Kuwastanisha muda wa kazi Kwa makubaliano ya pamoja baina ya Chama cha Wafanyakazi na mwajiri muda wa kazi unaweza kupangwa kutegemea mahitaji ya mwajiri na bila kujali kizuizi cha muda wa kazi wa saa 12 kwa siku. Mfanyakazi katika utaratibu huu atafanya kazi kwa muda usiozidi saa 40 kwa wiki na saa za ziada zisizozidi 10 kwa wiki. Makubaliano hayo ya pamoja yanapaswa yasizidi mwaka mmoja. Chini ya utaratibu huu muda wa kazi unaweza kutofautiana katika wiki mbalimbali ili mradi saa za kufanya kazi zisizidi ukomo uliowekwa kisheria. Mfano Chama cha Wafanyakazi na Mwajiri wanaweza kukubaliana kuwastanisha muda kwa kipindi cha miezi sita. Hivyo basi muda wa kazi kwa kipindi cha miezi hiyo sita kitakuwa saa za kazi za kawaida x wiki 4 x miezi 6 = 40 x 4 x 6= 960 Kwa hiyo Mwajiri anaweza kupanga muda wa kazi kulingana na mahitaji yake ndani ya mzunguko wa miezi sita kwa kuwataka wafanyakazi wafanye kazi kwa muda mrefu katika baadhi ya wiki na muda mfupi katika baadhi ya wiki. Kitu cha msingi ni kuhakikisha wafanyakazi hawafanyi kazi kwa zaidi ya saa za kawaida 40 kwa wiki na saa za ziada 10 kwa wiki. Kazi za Usiku Kazi za usiku ni zile zinazofanyika baada ya saa mbili kamili usiku na kabla ya saa 12 kamili alfajiri. Hairuhusiwi kwa Mwajiri kuwataka au kuwaruhusu kufanya kazi usiku wafanyakazi wafuatao: (a) Wajawazito ambao wamebakiza miezi miwili(2) kabla ya tarehe wanayotarajia kujifungua au kabla ya hapo kwa ushauri wa Daktari. (b) Wazazi miezi miwili(2) baada ya kujifungua au zaidi ya hapo kwa ushauri wa Daktari. 13 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (c) Watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane(18). (d) Mfanyakazi yeyote mwenye uthibitisho toka kwa Daktari kuwa hawezi kufanya kazi usiku. Mfanyakazi aliyefanya kazi usiku anastahili kulipwa posho ya kufanya kazi usiku ya angalau asilimia tano(5%) ya mshahara wake wa saa kwa kila saa aliyofanya kazi usiku. Mfanyakazi mshahara wake ni Tsh. 150,000/= kwa mwezi amefanya kazi usiku kwa siku tano katika mwezi na katika kila siku aliyofanya kazi usiku alifanya kazi kwa saa nane. Je! Atapata shilingi ngapi posho ya kufanya kazi usiku? 1: Tafuta mshahara wa saa: = 150,000 4.333 x 45 = 150,000= 769/20 195 2: Tafuta Saa alizofanya kazi usiku: = Saa 8 x 5= 40 3: Tafuta Posho ya Usiku: = 769/20 x 40 x 5= 1,538.40 100 Mapumziko ya Siku Mwajiri ni lazima ampe mfanyakazi mapumziko ya angalau saa 12 mfululizo kati ya muda anaomaliza kazi na muda atakaoanza kazi siku inayofuata. Muda wa mapumziko unaweza kupungua hadi kufikia saa 8 kwa makubaliano ya maandishi pale ambapo mfanyakazi atapata mapumziko ya angalau saa 3 katikati ya saa za kazi za kawaida au pale ambapo mfanyakazi anaishi katika eneo la kazi. 14 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Mapumziko ya Wiki Mwajiri ni lazima ampe mfanyakazi mapumziko ya angalau saa 24 mfululizo kati ya siku ya kawaida ya mwisho katika wiki na siku ya kwanza ya kazi ya kawaida ya wiki inayofuatia. Muda huu wa mapumziko unajumuisha Jumapili isipokuwa pale ambapo kuna makubaliano yanayoelekeza vinginevyo. Kwa makubaliano ya maandishi muda wa mapumziko ya wiki unaweza kuongezwa hadi kufikia saa 60 mfululizo kila baada ya wiki mbili au muda wa mapumziko kupunguzwa hadi kufikia saa 8 katika wiki yoyote iwapo muda wa mapumziko katika wiki inayofuata utaongezwa kwa kiwango sawa. Mfanyakazi atafanya kazi siku ya mapumziko kwa makubaliano na mwajiri ni lazima amlipe mara mbili ya mshahara wake wa saa kwa kila saa atakayofanya kazi siku ya mapumziko. Mapumziko ya Chakula Mwajiri ni lazima ampe mfanyakazi mapumziko ya angalau dakika sitini(60) mfululizo kwa ajili ya kupata chakula pale mfanyakazi anapofanya kazi mfululizo kwa kipindi kisichopungua saa tano(5). Wakati wa mapumziko kwa ajili ya chakula mfanyakazi anaweza kuendelea na kazi iwapo kazi hiyo haiwezi kuachwa au kufanywa na mtu mwingine na anapaswa kulipwa. UJIRA Mfanyakazi anastahili kulipwa mshahara usiopungua kima cha chini cha mishahara kilichopangwa kisheria. Mshahara utapangwa kwa kuzingatia saa za kazi za kawaida na kwa msingi wa jedwali la pili la sheria; (a) Mshahara wa mwezi gawa kwa 4.333 ni sawa na mshahara wa wiki. (b) Mshahara wa wiki gawa kwa saa za kazi za kawaida katika wiki ni sawa na mshahara wa siku. 15 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (c) Mshahara wa siku gawa kwa saa za kazi za kawaida katika siku ni sawa na mshahara wa saa. (d) Endapo mfanyakazi analipwa mshahara kwa vigezo vingine tofauti na kigezo cha saa za kazi, itachukuliwa kuwa mfanyakazi huyo analipwa mshahara kwa wiki kwa utaratibu ufuatao: (i) Jumla ya kiasi alicholipwa katika kipindi cha wiki 13 kabla ya siku ya malipo gawa kwa 13; au (ii) Kama amefanya kazi pungufu ya wiki 13, jumla ya kiasi alicholipwa gawa kwa wiki alizofanya kazi kabla ya malipo. Mshahara ni lazima ulipwe a) Wakati wa saa za kazi. b) Mahali pa kazi. c) Katika siku iliyokubalika kuwa siku ya malipo. d) Kwa kuwekwa kwenye bahasha iliyofungwa. e) Kwa kuzingatia kipindi cha malipo yaani siku, wiki, wiki mbili au mwezi kwa mujibu wa mkataba wa mfanyakazi. Mwajiri ni lazima atoe'salary slip' MAKATO Mwajiri anaruhusiwa kukata makato yafuatayo kutoka mshahara wa mfanyakazi: a) Kwa mujibu wa Sheria kama vile Kodi, Michango ya Pensheni, n.k. b) Kwa amri ya Mahakama au Tuzo ya Mwamuzi. c) Marejesho ya Mkopo iwapo mfanyakazi ameelekeza au kuridhia kwa maandishi. d) Ada ya Chama cha Wafanyakazi baada ya kutoa idhini kwa Fomu TUF. 6. 16 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Kila mfanyakazi analo jukumu la kutunza mali za mwajiri, endapo mfanyakazi ataharibu mali za mwajiri kwa uzembe, mwajiri anaweza kumkata mfanyakazi mshahara wake kufidia hasara iliyotokea. Hata hivyo kabla ya kuchukua hatua hiyo mwajiri anapaswa kuhakikisha kuwa: a) Anazingatia utaratibu wa haki. b) Hasara au uharibifu umetokea wakati mfanyakazi akiwa kazini na kwa sababu ya kosa la mfanyakazi. c) Anampa mfanyakazi maelezo ya maandishi ya kiasi cha deni, chanzo cha uharibifu au hasara na hesabu za namna deni hilo lilivyofikiwa. d) Mfanyakazi anapewa nafasi ya kujitetea na kupinga deni hilo, chanzo na namna hesabu za deni hilo zilivyofikiwa. e) Jumla ya deni isizidi kiwango halisi cha hasara au uharibifu. f) Makato yasizidi robo ya mshahara wa mfanyakazi. LIKIZO Wafanyakazi wafuatao wanastahili likizo ya malipo: (a) Waliofanya kazi kwa zaidi ya miezi sita mfululizo. (b) Wafanyakazi wa msimu. (c) Wafanyakazi waliofanya kazi kwa kipindi tofauti kwa mwajiri mmoja katika mwaka iwapo vipindi husika vikijumlishwa vitazidi miezi sita. Mfanyakazi ana haki ya kupata likizo zifuatazo: a) Likizo ya mwaka. b) Likizo ya uzazi kwa akina mama. c) Likizo ya ugonjwa. 17 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania d) Likizo ya Uzazi kwa akina baba e) Likizo ya huruma au majukumu ya kifamilia. Likizo ya mwaka mzunguko wake ni miezi 12 na likizo nyingine zilizobaki mzunguko wake ni miezi 36. Likizo ya mwaka a) Mfanyakazi anastahili kupewa likizo ya siku 28 mfululizo katika mzunguko wa miezi 12. b) Siku za likizo zinaweza kukatwa na mwajiri iwapo mfanyakazi alipewa ruhusa mbalimbali. c) Mwajiri anaweza kuamua siku ya kuanza likizo mfanyakazi ndani ya miezi sita kuanzia siku ambayo mfanyakazi alistahili kuanza likizo. d) Muda wa kuanza likizo baada ya miezi 6 unaweza kuongezwa kwa makubaliano iwapo yapo mahitaji ya uendeshaji na nyongeza ya muda wa kuanza likizo isizidi miezi 12. e) Mfanyakazi hapaswi kufanya kazi wakati wa likizo. f) Hairuhisiwi kumlipa mfanyakazi pesa badala ya likizo(kununua likizo) isipokuwa tu wakati wa kusitisha ajira. g) Likizo ya mwaka haitakiwi kuchukuliwa wakati wa likizo nyingine au wakati wa kipindi cha notisi ya kusitisha ajira. h) Mwajiri ni lazima amlipe mfanyakazi mshahara wake wakati wa likizo. i) Mwajiri ni lazima amlipe mfanyakazi malipo mengine yanayoambatana na likizo kwa mujibu wa Tamko au Amri ya kima cha chini cha mshahara na masharti ya ajira. 18 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Likizo ya Uzazi kina mama a) Mfanyakazi anastahili likizo ya uzazi ya malipo ya siku themanini na nne(84) au siku mia moja(100) iwapo atajifungua mtoto zaidi ya mmoja katika mzunguko wa miezi 36. b) Mfanyakazi analo jukumu la kutoa notisi ya ujauzito kwa mwajiri miezi mitatu kabla ya tarehe anayotarajia kujifungua. NOTISI hiyo inapaswa iambatane na uthibitisho kutoka kwa Daktari. c) Mfanyakazi anaweza kuanza likizo ya uzazi wiki nne kabla ya tarehe anayotarajia kujifungua au kabla ya hapo kwa uthibitisho wa Daktari. d) Mfanyakazi anaweza kuanza kazi wiki sita baada ya kujifungua. Isipokuwa kama daktari atathibitisha kuwa anaweza kuanza kazi kabla ya muda huo kumalizika, e) Mwajiri anakatazwa kumtaka au kumruhusu mfanyakazi mjamzito au anayenyonyesha kufanya kazi zenye madhara kwa afya ya mfanyakazi huyo au afya ya mtoto wake. f) Endapo kazi za kawaida za mfanyakazi zina madhara kwa afya yake au ya mtoto wake, mwajiri ni lazima amtafutie kazi nyingine kwa masharti yale yale ya ajira yake. g) Mfanyakazi anastahili kupewa saa mbili(2) kila siku kwa ajili ya kunyonyesha. h) Mwajiri anawajibika kutoa likizo ya malipo ya uzazi kwa vipindi vinne (4) tu. i) Endapo mtoto aliyezaliwa atafariki ndani ya mwaka mmoja tangu kuzaliwa, na mfanyakazi akapata mtoto mwingine ndani ya mzunguko huohuo wa likizo, mfanyakazi atastahili kupata likizo nyingine ya malipo ya siku themanini na nne(84). j) Ni kinyume cha Sheria kumwachisha kazi mfanyakazi kwa sababu ya ujauzito au majukumu ya kifamilia. k) Mfanyakazi aliyemaliza likizo ya uzazi ataendelea na ajira yake kwa masharti yaleyale ya ajira yake. 19 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Likizo ya Uzazi ya kina baba a) Mfanyakazi anastahili angalau siku tatu(3) za likizo ya uzazi ya baba katika mzunguko wa miezi thelathini na sita(36) bila kujali idadi ya matukio. b) Mfanyakazi atapoteza haki za likizo endapo atashindwa kuchukua likizo hiyo ndani ya siku saba(7) baada ya mtoto kuzaliwa. c) Mfanyakazi analo jukumu la kuthibitisha mtoto aliyezaliwa ni wake. Likizo ya Ugonjwa a) Mfanyakazi anastahili likizo ya ugonjwa ya angalau siku 126 katika mzunguko wa miezi 36. b) Katika siku 63 za kwanza mfanyakazi anastahili kulipwa mshahara kamili na katika siku 63 zinazofuata anastahili kulipwa nusu mshahara. c) Kabla ya kuchukua likizo ya ugonjwa mfanyakazi anapaswa kuwasilisha kwa Mwajiri uthibitisho wa Daktari. d) Endapo mfanyakazi anastahili kulipwa wakati wa likizo ya ugonjwa kwa mujibu wa Sheria, mfuko wowote au makubaliano ya pamoja, Mwajiri atakuwa hana jukumu la kumlipa mfanyakazi huyo wakati wa likizo. Likizo ya Huruma au Majukumu ya Kifamilia Mfanyakazi anastahili angalau siku nne(4) za likizo ya malipo katika mzunguko wa miezi 36 bila kujali idadi ya matukio kwa sababu zifuatazo: (i) Kuugua au kifo cha mtoto. (ii) Kifo cha mke/mume, mzazi, babu, bibi, mjukuu au ndugu wa kuzaliwa. Mfanyakazi anaweza kupewa siku zaidi ya nne(4) na mwajiri kwa tukio moja au matukio mengine katika mzunguko wa likizo, siku ambazo zinaweza kupunguzwa katika likizo ya mwaka au kutolipwa mshahara wa siku hizo. Angalizo: Siku za likizo zinaweza kuongezwa kupitia makubaliano ya pamoja au kanuni za mwajiri. 20 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania SURA YA TANO USITISHAJI AJIRA Usitishaji ajira ni kukoma kwa mkataba wa ajira, kutokana na sababu mbalimbali kama vile; kujiuzulu au kuacha kazi mfanyakazi, mfanyakazi kuachishwa kazi na mwajiri wake kwa kupewa au kutokupewa NOTISI, kutorejewa mkataba wa muda maalum kwa mfanyakazi anayetarajia mkataba huo kurejewa, kukataliwa na Mwajiri kuanza kazi baada ya likizo ya uzazi, mfanyakazi kushindwa kuendelea na ajira baada ya mwajiri kujenga mazingira magumu kwa mfanyakazi kuendelea na kazi, kuachishwa kazi kwa sababu ya utovu wa nidhamu, uwezo mdogo wa kufanya kazi, kutohitajika, mahitaji ya uendeshaji ya mwajiri, kwa makubaliano, kwa kumaliza kazi maalum, kwa tukio litakalofanya vigumu kuendelea na mkataba, kifo, n.k. Usitishaji ajira usio halali Usitishaji ajira kwa sababu zifuatazo si halali: a) Mfanyakazi kutoa taarifa ambazo anapaswa kuzitoa kwa mujibu wa sheria. b) Mfanyakazi kushindwa au kukataa kufanya jambo lolote linalokatazwa na sheria. c) Mfanyakazi kutekeleza haki zake kwa mujibu wa sheria. d) Mfanyakazi kuwa mwanachama wa Chama cha Wafanyakazi. e) Mfanyakazi kushiriki katika shughuli halali za Chama cha Wafanyakazi ikiwemo mgomo halali. f) Ulemavu g) Ujauzito h) Ubaguzi. 21 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Usitishaji ajira kwa uonevu Mwajiri atakayeshindwa kuthibitisha mambo yafuatayo hapa chini anapositisha ajira ya mfanyakazi atakuwa amemwachisha mfanyakazi huyo kwa uonevu. Mambo hayo ya msingi kuthibitisha ni: a) Sababu za kusitisha ajira ni halali. b) Sababu za kusitisha ajira ni za haki kwa maana zinahusiana na utovu wa nidhamu, uwezo mdogo wa kufanya kazi, kutohitajika, mahitaji ya uendeshaji ya Mwajiri. c) Utaratibu uliotumika kusitisha ajira umezingatia misingi ya haki. Usitishaji ajira kwa sababu ya utovu wa nidhamu Utovu wa nidhamu ni moja ya sababu zinazoweza kusababisha Mwajiri amuachishe kazi mfanyakazi. Hatua za nidhamu zinapaswa zichukuliwe hatua kwa hatua kwa madhumuni ya kurekebisha tabia ya mfanyakazi badala ya kuadhibu. Mwajiri anapaswa kutoa ushauri nasaha, onyo la mdomo, onyo la maandishi pale ambapo mfanyakazi anaendeleza utovu wa nidhamu. Kuachisha kazi kunapaswa kuwe hatua ya mwisho kabisa katika kusimamia nidhamu mahali pa kazi. Mwajiri anapaswa kuweka kanuni za nidhamu zinazoeleza namna wafanyakazi wanavyopaswa kutunza nidhamu mahali pa kazi. Mwajiri anapaswa kuwafahamisha wafanyakazi wote kuhusu kanuni hizo wakati wa kuajiri, wakati wa vikao au kubandika katika mbao za matangazo, ni vizuri iwapo kila mfanyakazi atapatiwa nakala yake. Kanuni za utendaji mzuri zimeweka mwongozo wa namna ya kusitisha ajira kwa haki. Kila mwajiri anapaswa kuzingatia mwongozo huo ambao unaanisha mambo makuu mawili ya kuzingatia sababu za kusitisha ajira na utaratibu ambao Mwajiri anapaswa kuzingatia wakati wa kusitisha ajira. Sababu a) Lazima ziwepo sababu halali za kusitisha ajira kwa mfano: wizi, shambulio, n.k. 22 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania b) Sababu zisiwe sababu zinazokatazwa na sheria kwa mfano: ujauzito, ulemavu, n.k. Kabla ya kumwachisha kazi mfanyakazi mwajiri ni lazima afikirie kwa makini na kuangalia endapo: a) Mfanyakazi amekiuka Kanuni za Nidhamu. b) Kanuni iliyokiukwa ni ya haki. c) Mfanyakazi alikuwa anafahamu kanuni aliyoikiuka. d) Kanuni iliyokiukwa inaeleweka na haina utata. e) Kanuni iliyokiukwa imekuwa ikitumika kwa usawa kwa wafanyakazi. f) Adhabu ya kuachishwa kazi ndiyo muafaka kwa kosa lililotendwa. Kosa la kwanza halihalalishi adhabu ya kuachisha kazi isipokuwa pale itakapothibitika kosa ni kubwa kiasi cha kuharibu uhusiano wa kiajira kiasi cha kutovumilika. Makosa makubwa yanayoweza kuhalalisha mfanyakazi kuachishwa kazi kwa kosa la kwanza ni: a) Kukosa uaminifu kulikokithiri kama vile kughushi, wizi, n.k. b) Kuharibu mali kwa kukusudia. c) Kuhatarisha usalama wa watu wengine kwa makusudi. d) Uzembe uliokithiri. e) Kushambulia. f) Ukaidi uliokithiri. Hata hivyo kabla ya kuchukua hatua ya kumwachisha kazi mfanyakazi kwa makosa makubwa Mwajiri anapaswa aangalie kwa makini mazingira ya kosa lilivyotendeka, aina ya kazi, afya na usalama na uwezekano wa kosa kurudiwa. Mwajiri anapaswa azingatie pia, utendaji wa mfanyakazi, kumbukumbu za utumishi wake, kwa maana ya rekodi yake ya utumishi, muda wa utumishi, rekodi yake ya nidhamu na hali yake binafsi. 23 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Utaratibu wa Haki Kabla ya kuchukua hatua za nidhamu dhidi ya mfanyakazi, Mwajiri ni lazima afanye uchunguzi wa awali kuona iwapo ipo haja ya kuitisha kikao cha nidhamu. Endapo Mwajiri ataona ipo haja ya kuitisha kikao cha nidhamu anapaswa afanye mambo yafuatayo: a) Kumpa taarifa mfanyakazi ya tuhuma kwa namna ambayo atazielewa kikamilifu tuhuma hizo. b) Mfanyakazi apewe muda wa kutosha kuandaa utetezi kwa kuzingatia uzito wa kosa. Muda huo usipungue saa 48. c) Mfanyakazi aelezwe waziwazi haki yake ya kuwakilishwa na mfanyakazi mwenzake au kiongozi wake wa Chama mahali pa kazi. d) Ateue Mwenyekiti wa Kikao ambae hajahusika na suala lililosababisha kikao kiitishwe kusikiliza shauri hilo. e) Mfanyakazi apewe fursa ya kuita mashahidi na kuwahoji kwa kuwadodosa mashahidi wa Mwajiri. f) Endapo matokeo ya kikao yatakuwa kupatikana na hatia mfanyakazi adhabu isitolewe papo hapo. Nafasi itolewe kwa mfanyakazi kutoa hoja za kupunguziwa adhabu kabla ya adhabu kutolewa. g) Endapo mfanyakazi anayetuhumiwa ni kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi katika ngazi yoyote, Mwajiri ni lazima atoe nafasi kwa kiongozi huyo kuwakilishwa na mtendaji wa Chama katika kikao cha nidhamu. h) Endapo adhabu inayotolewa ni kuachishwa kazi Mwajiri ni lazima atoe sababu na aeleze haki ya mfanyakazi kukata rufaa ngazi ya juu au kupeleka rufaa yake Tume ya Usuluhishi na Uamuzi. i) Mfanyakazi ni lazima apewe nakala ya fomu ya kusikiliza shauri baada ya kikao cha nidhamu. 24 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Usitishaji ajira kwa sababu ya uwezo mdogo wa kazi Uwezo wa mfanyakazi unaweza kupungua kutokana na ugonjwa, kuumia au utendaji usioridhisha. Kila sababu inapaswa kushughulikiwa kwa namna ya pekee. Utendaji usioridhisha Sheria inatambua haki ya mwajiri kuweka viwango vya kazi, viwango ambavyo wafanyakazi wanapaswa kuzingatia katika utendaji wao ili mradi viwango hivyo ni vya haki na vinavyotekelezeka na kufahamika kwa wafanyakazi. Upimaji utendaji wa mfanyakazi Iwapo utendaji wa mfanyakazi hauridhishi, mwajiri anapaswa kufanya yafuatayo: a) Kumpa taarifa mfanyakazi kwamba utendaji wake haufikii viwango vilivyowekwa. b) Kumpa mfanyakazi maelekezo, mafunzo na miongozo kwa lengo la kuboresha utendaji. c) Kufanya vikao vya mara kwa mara na mfanyakazi pamoja na kumpa ushauri. d) Kutoa fursa na muda wa kutosha kwa mfanyakazi kuboresha utendaji wake. Iwapo utendaji wa mfanyakazi utakuwa hauridhishi hata baada ya kupewa muda wa kutosha, mwajiri ni lazima amwandikie mfanyakazi kumweleza mambo yafuatayo: a) Kwamba utendaji wake bado hauridhishi na hajafikia viwango vinavyotakiwa. b) Kwamba anaweza kuachishwa kazi iwapo hataboresha utendaji wake Mwajiri anapaswa kufanya uchunguzi kwa madhumuni ya kubaini: 25 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania N Sababu za utendaji usioridhisha. N Endapo upo uwezekano wa kumbadilishia kazi mfanyakazi au kumwondolea baadhi ya majukumu. Wakati wa uchunguzi, Mwajiri ni lazima amshirikishe mfanyakazi pamoja na mwakilishi wake ambaye anaweza kuwa mfanyakazi mwenzake au kiongozi wake wa Chama mahali pa kazi. Endapo Mwajiri ataamua kumwachisha kazi mfanyakazi kwa sababu ya utendaji usioridhisha mwajiri ni lazima aitishe kikao ambapo: N Mfanyakazi atapewa tuhuma. N Mfanyakazi atapewa nafasi ya kujitetea. N Mfanyakazi atawakilishwa na mfanyakazi mwenzake au kiongozi wa Chama mahali pa kazi. Katika kikao hicho mwajiri anapaswa kuangalia njia mbadala tofauti na kumwachisha kazi mfanyakazi. Usitishaji ajira kwa wafanyakazi waliopo katika kipindi cha majaribio Madhumuni ya kuwekwa kipindi cha majaribio ni kupima uwezo wa mfanyakazi kuona kama anafaa kwa kazi alioyoajiriwa kufanya. Kipindi cha majaribio kinapaswa kisiwe kirefu sana na kisizidi miezi kumi na mbili kwa kuzingatia aina ya kazi. Viwango vya utendaji vinavyotakiwa na utamaduni na mazoea ya sekta husika. Wakati wa kipindi cha majaribio mwajiri anapaswa kukutana na mfanyakazi mara kwa mara kupima utendaji na kujadiliana naye ikiwezekana kumpa miongozo mbalimbali, mafunzo na ushauri. Mwajiri kwa kushauriana na mfanyakazi anaweza kuongeza muda wa majaribio. Endapo katika kipindi cha majaribio mwajiri ataona utendaji wa mfanyakazi hauridhishi mwajiri anaweza kusitisha ajira. Kabla ya kuchukua hatua ya kusitisha ajira mwajiri ni lazima: 26 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania a) Amtaarifu mfanyakazi akieleza kutoridhishwa na utendaji wake. b) Ampe mfanyakazi nafasi ya kujibu na kujitetea dhidi ya tuhuma hiyo. c) Awe amempa muda wa kutosha mfanyakazi kuboresha utendaji wake au tabia na mfanyakazi kushindwa. d) Ampe nafasi ya kuwakilishwa na mfanyakazi mwenzake au kiongozi wa Chama mahali pa kazi katika mchakato wote. Usitishaji ajira kwa sababu ya ugonjwa au kuumia Ugonjwa na kuumia inaweza kuwa sababu ya kusitisha ajira. Kabla ya mwajiri kuchukua hatua hiyo ni lazima afanye uchunguzi wa kina kubaini mambo yafuatayo: a) Chanzo cha ugonjwa au kuumia. b) Kiwango cha ugonjwa au kuumia. c) Endapo ugonjwa au matokeo ya kuumia ni ya muda au ya kudumu. Katika kubaini mambo hayo mwajiri ni lazima aongozwe na maoni ya Daktari aliyesajiliwa. Endapo itabainika kuwa chanzo cha ugonjwa au kuumia kunatokana na kazi jukumu la Mwajiri kuendeleza ajira ya mfanyakazi ni kubwa. Mambo mengine ya kuchunguza kabla ya kusitisha ajira ni: d) Kuangalia uwezekano wa kuendeleza ajira ya mfanyakazi katika hali aliyonayo. e) Kuwepo kwa mfuko wa fidia kwa mfanyakazi au pensheni. 27 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Ugonjwa wa kudumu au matokeo kudumu ya kuumia Endapo ugonjwa utakuwa wa kudumu au matokeo ya kuumia ni ya kudumu Mwajiri anapaswa kufikiria hatua tofauti na kusitisha ajira kama vile:a) Kumbadilishia mfanyakazi kazi. b) Kumsaidia mfanyakazi kufanya kazi katika hali ya ulemavu aliyonayo. Kama uwezekano huo haupo basi mwajiri anaweza kusitisha ajira. Ugonjwa wa muda au matokeo ya muda ya kuumia Endapo itabainika kuwa mfanyakazi atakuwa nje ya kazi kwa muda mrefu, mwajiri ni lazima achunguze na aangalie namna atakavyoendeleza ajira ya mfanyakazi badala ya kusitisha ajira kwa kufanya yafuatayo: a) Kumbadilishia kazi mfanyakazi kwa muda. b) Kumpa mfanyakazi kazi nyepesi c) Kumpa mfanyakazi kazi mbadala. d) Kumpa mfanyakazi nafasi ya kustaafu mapema. Mambo ya msingi kwa mwajiri kuzingatia katika uchunguzi wake ni pamoja na: a) Aina ya kazi. b) Muda ambao mfanyakazi atakosekana kazini. c) Kiwango cha ugonjwa au kuumia. d) Uwezekano wa kumbadilishia kazi mfanyakazi kwa muda au kumsaidia mfanyakazi kufanya kazi katika hali aliyonayo. 28 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Endapo chanzo cha tatizo ni matumizi mabaya ya madawa na kilevi, ushauri nasaha na kumrekebisha mfanyakazi ndiyo hatua sahihi kwa mwajiri kufikiria na kuchukua. HIV/UKIMWI Hairuhusiwi kusitisha ajira ya mfanyakazi kwa sababu ya HIV/UKIMWI, mfanyakazi mwenye tatizo hilo ni lazima aendelee na kazi kwa masharti yake ya kawaida ya kazi kwa kadri afya yake itakavyoruhusu. Endapo itatokea mfanyakazi huyo kushindwa kuendelea na kazi zake za kawaida, Mwajiri ni lazima ambadilishie kazi bila kuathiri ujira wake. Pale ambapo mfanyakazi atakuwa mgonjwa kiasi cha kushindwa kuendelea na ajira, basi utaratibu wa haki wa kusitisha ajira ni lazima ufuatwe. Mfanyakazi ni lazima ashirikishwe na kushauriana naye wakati wote wa mchakato wa kubaini chanzo, kiwango, n.k. cha ugonjwa au kuumia na ni haki yake kuwakilishwa na mfanyakazi mwenzake au kiongozi wake wa Chama mahali pa kazi wakati wa mchakato huo. Kabla ya kufikia uamuzi wa kusitisha ajira ya mfanyakazi kwa sababu ya ugonjwa au kuumia Mwajiri ni lazima aitishe kikao kati yake na mfanyakazi akiwa na mwakilishi wake. Katika kikao hicho Mwajiri ataeleza sababu zake za kutaka kusitisha ajira na kutoa nafasi kwa mfanyakazi na mwakilishi wake kubeza sababu hizo, na kutoa hoja zao. Mwajiri ni lazima azingatie hoja zilizotolewa na mfanyakazi na mwakilishi wake na kama anazikataa atoe sababu. Mfanyakazi ni lazima afahamishwe matokeo ya kikao kwa maandishi. Usitishaji ajira kwa sababu ya kutohitajika Kutohitajika ni moja ya sababu za kusitisha ajira. Kuna aina mbili za kutohitajika: a) Mfanyakazi kutofaa katika kazi kwa sababu ya tabia au hulka yake. b) Mfanyakazi kuwa na uhusiano mbaya na wafanyakazi wenzake, wateja, au watu wengine muhimu kwa shirika. 29 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Kabla ya kuchukua hatua ya kusitisha ajira mwajiri ni lazima: a) Aweke kumbukumbu za matukio aliyoyafanya mfanyakazi husika na kusababisha matatizo au kuvurugika kazi. b) Amuonye na kumshauri mfanyakazi au kupendekeza hatua za kurekebisha hali hiyo kabla ya kusitisha ajira. Kabla ya kuchukua hatua ya kusitisha ajira, Mwajiri ni lazima atoe fursa ya haki kwa mfanyakazi: a) Kutafakari na kujibu tuhuma. b) Kuondoa chanzo cha tatizo. c) Kupendekeza njia mbalimbali tofauti na kusitisha ajira. Usitishaji wa ajira kwa sababu ya mahitaji ya uendeshaji Mahitaji ya uendeshaji ya Mwajiri ni moja ya sababu za kusitisha ajira. Mahitaji ya uendeshaji ya Mwajiri, yamegawanyika katika mafungu makuu matatu yafuatayo: a) Mahitaji ya kiuchumi yanayohusiana na usimamizi wa fedha. b) Mahitaji ya teknoklojia kwa maana ya kupatikana teknolojia mpya inayosababisha baadhi ya wafanyakazi kutokuwa na kazi za kufanya. c) Mahitaji ya kubadili mpangilio wa shughuli za Shirika kutokana na kuunganisha biashara, mabadiliko ya biashara, n.k. Mashauriano Mwajiri kabla ya kusitisha ajira za wafanyakazi kwa sababu ya mahitaji ya uendeshaji(kupunguza) ni lazima afanye mashauriano na wafanyakazi kupitia Chama cha Wafanyakazi au moja kwa moja na wafanyakazi iwapo hakuna Chama cha Wafanyakazi. 30 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Madhumuni ya kushauriana na kuziwezesha pande zote husika kufikia makubaliano kuhusu: a) Sababu za kupunguza wafanyakazi. b) Hatua za kuzuia upunguzaji au kupunguza idadi ya watakaopunguzwa kama vile kuwahamishia kwenye kazi nyingine baadhi ya wafanyakazi, kustaafu mapema, kupunguzwa kwa hiari, likizo bila malipo, n.k. c) Vigezo vya kuchagua watakaopunguzwa kama vile(LIFO), uzoefu, stadi maalum, sifa, upendeleo maalum, n.k. d) Muda wa zoezi la kupunguza wafanyakazi. e) Kiinua mgongo. f) Hatua za kupunguza makali ya kukosa kazi kama vile kupewa muda wa kutafuta kazi nyingine. Utoaji wa taarifa Kabla ya mchakato wa mashauriano kuanza Mwajiri anapaswa kutoa taarifa muhimu kwa Chama cha Wafanyakazi au Wafanyakazi kwa maandishi akieleza: a) Sababu za kupunguza. b) Hatua mbadala za kuzuia au kupunguza idadi ya watakaopunguzwa na kwa nini haziwezekani. c) Idadi ya wafanyakazi anaokusudia kuwapunguza na kazi zao. d) Mapendekezo ya vigezo vitakavyotumika. e) Muda wa zoezi. f) Mapendekezo ya kiinua mgongo. g) Msaada atakaotoa mwajiri kwa watakaopunguzwa. 31 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Fursa ya mlishonyuma Mchakato wa mashauriano ni lazima utoe nafasi kwa Chama cha Wafanyakazi au Wawakilishi wa Wafanyakazi: a) Kukutana na kuwataarifu wafanyakazi maendeleo ya mashauriano. b) Kukutana na Mwajiri na c) Kuomba, kupokea na kuchambua taarifa muhimu kukiwezesha Chama au Wawakilishi wa Wafanyakazi kuelewa kwa ufasaha taarifa hizo na kushauriana na Mwajiri kwa madhumuni ya kufikia makubaliano kuhusu hatua mbalimbali za kushughulikia zoezi hilo. Usuluhishi Endapo hakuna makubaliano yoyote, suala hilo litapelekwa mbele ya Tume kwa usuluhishi. Katika kipindi cha usuluhishi cha siku 30 Mwajiri haruhusiwi kupunguza. Siku 30 zikipita bila makubaliano yoyote kufikiwa, Mwajiri anaweza kuwapunguza kazi wafanyakazi. Upendeleo wa kuajiriwa upya Wafanyakazi watakaopunguzwa watapewa upendeleo wa kuajiriwa kwanza endapo zitatokea nafasi ili mradi wawe na sifa zinazotakiwa na mfanyakazi awe alieleza nia ya kuajiriwa upya nafasi ikitokea na yapo makubaliano ya pamoja baina ya Mwajiri na Chama. Usitishaji ajira kwa kutoa taarifa Upande wowote baina ya Mwajiri na mfanyakazi, unaweza kusitisha mkataba wa ajira kwa kutoa taarifa(notisi) ya maandishi ikieleza sababu za kusitisha ajira na tarehe ya kutolewa taarifa hiyo. Muda wa taarifa ya kusitisha ajira unapaswa usipungue: a) Siku saba(7) iwapo taarifa itatolewa katika mwezi wa kwanza wa ajira. b) Kwa mfanyakazi aliyefanya kazi zaidi ya mwezi: 32 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (i) Siku nne(4) iwapo mfanyakazi analipwa mshahara wake kila siku au kila wiki. (ii) Siku ishirini na nane(28) iwapo mfanyakazi analipwa mshahara wake kila mwezi. Muda wa taarifa unaweza kuongezwa kwa makubaliano. Hairuhusiwi kutoa taarifa ya kusitisha ajira wakati wa likizo au kutoa taarifa hiyo sambamba na likizo. Mwajiri anaweza kusitisha ajira ya mfanyakazi na kumlipa mshahara badala ya taarifa. Mfanyakazi anayo haki ya kukata rufaa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi endapo hajaridhika na hatua ya Mwajiri kusitisha ajira kwa taarifa au kwa malipo badala ya taarifa. Kusimamishwa kazi Mwajiri anaweza kumsimamisha kazi mfanyakazi kwa sababu kuu mbili: a) Kupisha uchunguzi pale ambapo mfanyakazi anakabiliwa na tuhuma za nidhamu au uwezo mdogo wa kazi. b) Adhabu kwa kosa la utovu wa nidhamu, ili mradi kusimamishwa kazi hakutazidi siku thelathini(30). Mfanyakazi anayesimamishwa kazi kupisha uchunguzi anastahili kulipwa mshahara wake kamili pamoja na marupurupu yake. Mfanyakazi anayeadhibiwa kwa kusimamishwa kazi hastahili kulipwa mshahara kwa kipindi atakachosimamishwa kazi. Nafuu anazostahili mfanyakazi aliyeachishwa kazi kwa uonevu Mahakama au Mwamuzi, wakithibitisha kuwa mfanyakazi aliachishwa kazi kwa uonevu, wanaweza kuamuru: a) Mfanyakazi arejeshwe kazini bila masharti yoyote; au 33 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania b) Mfanyakazi aajiriwe upya kwa masharti yoyote yatakayowekwa na Mahakama au mwamuzi; au c) Mfanyakazi alipwe fidia isiyopungua mishahara ya miezi kumi na mbili. Mwajiri anapoamua kutomrejesha kazini au kutomuajiri upya mfanyakazi Mwajiri akiamua kutomrejesha kazini au kutomuajiri upya mfanyakazi kama alivyoamuriwa na Mahakama au Mwamuzi, anapaswa kumlipa mfanyakazi huyo mafao yake yote na haki zake zote ikijumuisha mishahara yake kuanzia siku aliyoachishwa kazi kwa uonevu hadi siku ya malipo, pamoja na mishahara ya miezi kumi na mbili(12). Malipo ya Kisheria mfanyakazi anapoachishwa kazi Mfanyakazi aliyeachishwa kazi, anastahili kulipwa malipo yafuatayo: a) Mshahara badala ya taarifa kama hakupewa taarifa. b) Mshahara kwa kazi aliyofanya kabla ya kuachishwa. c) Likizo ambazo hajaenda. d) Siku za likizo ambayo mzunguko wake haujakamilika. e) Kiinua mgongo, angalau mshahara wa siku saba kwa kila mwaka kamili ambao mfanyakazi amefanya kazi kwa mwajiri. Hata hivyo mfanyakazi aliyeachishwa kazi kwa utovu wa nidhamu au aliyeachishwa kazi kwa sababu ya uwezo, kutohitajika au mahitaji ya uendeshaji na kukataa ajira mbadala. f) Nauli yake na familia pamoja na mizigo mpaka mahali alipoajiriwa. Mfanyakazi aliyeachishwa kazi anastahili pia kupatiwa Cheti cha Utumishi. 34 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania SURA YA SITA UHURU WA KUJUMUIKA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI Uhuru wa kujumuika ni moja ya haki inayolindwa na Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini ambapo kila Mfanyakazi aliyeajirwa anayo haki ya kuunda na kujiunga na Chama cha Wafanyakazi pamoja na kushiriki katika shughuli halali za Chama chake. Hata hivyo uhuru huu umeweka mipaka kwa baadhi ya Wafanyakazi wafuatao:(a) Hakimu anaweza kuuunda au kujiunga na Chama cha Maafisa wa Mahakama pekee, (b) Mwendesha Mashitaka anaweza kuunda au kujiunga na Chama cha Waendesha mashitaka au watendaji wengine wa Mahakama pekee. (c) Mfanyakazi meneja Mwandamizi, ambaye kwa nafasi yake kazini anatengeneza sera kwa niaba ya Mwajiri na ana mamlaka ya kuingia katika makubaliano ya pamoja na Chama cha Wafanyakazi kwa niaba ya Mwajiri, anaweza asijiunge na Chama cha Wafanyakazi cha Wafanyakazi wasio Mameneja Waandamizi. Haki ya Uhuru wa kujumuika inatoa kinga ya kutobaguliwa kwa mfanyakazi anayetekeleza haki hii na kwa mtendaji au kiongozi wa Chama au Shirikisho, anapotekeleza majukumu yake halali. Hali kadhalika Chama chini ya haki ya Uhuru wa kujumuika kinakuwa na haki ya:(a) kutengeneza Katiba yake, (b) Kupanga na kuendesha mambo yake ya ndani na shughuli halali bila kuingiliwa. (c) Kujiunga au kuunda Shirikisho (d) Kushiriki katika shughuli halali za Shirikisho 35 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (e) Kujirishirikisha na Vyama au Mashirikisho ya kiulimwengu, kuchangia na kupokea misaada ya kifedha kutoka kwa vyama au mashirikisho hayo Utaratibu wa kuunda Chama cha Wafanyakazi Chama cha Wafanyakazi kinaanzishwa na Wafanyakazi wasiopungua 20. Wafanyakazi hao wanapaswa kuitisha kikao chao cha kuanzisha Chama, ambapo watajiorodhesha na kutia saini zao katika rejista ya mahudhurio. Watamteua Katibu wa Kikao ambaye atatayarisha muhtasari wa kikao wenye azimio la kuanzisha Chama. Katika kuanzisha Chama cha Wafanyakazi mambo yafuatayo ni lazima kuzingatiwa:(a) Chama kiwe ni Chama halisi cha Wafanyakazi (b) Kisiwe Chama kwa madhumuni ya kupata faida (c) Kiwe Chama huru kwa maana kisianzishwe na Mwajiri au Jumuiya ya Waajiri (d) Kianzishwe na Wafanyakazi wasiopungua 20 (e) Kiwe na Katiba na Kanuni zinazozingatia kifungu cha 47 cha Sheria; (f) Kiwe na jina lisilofanana na jina la Chama kingine, kuzuia mkanganyiko au kuwapotosha watu (g) Kiwe na makao yake makuu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Utaratibu wa kusajili chama Chama cha Wafanyakazi kinapaswa kujisajili ndani ya miezi sita kuanzia tarehe ya kuanzishwa kwake. 36 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Maombi ya usajili yatafanyika kwa kujaza fomu maalum ambayo itajazwa kikamilifu na kusainiwa na Katibu wa Kikao kilichoazimia kuanzisha Chama. Fomu hiyo ya maombi inapaswa kuambatana na nakala zilizothibitishwa za rejista ya mahudhurio, na muhtasari wa kikao kilichoanzisha Chama na nakala zilizothibitishwa za Katiba na Kanuni, na kuziwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Jumuiya za Waajiri. Msajili atakisajili Chama baada ya kuridhika kuwa kimetimiza masharti yote muhimu yaliyowekwa na Sheria. Iwapo Msajili hataridhika kwa maana ya Chama kushindwa kutimiza masharti ya Sheria anaweza kutoa nafasi ya kurekebisha kasoro au atakataa kusajili kwa kuwapa notisi waleta maombi, akieleza sababu za hatua yake hiyo. Asiyeridhika na uamuzi wa Msajili anayo haki ya kukata rufaa Mahakama ya Kazi. Wajibu wa Chama kilichosajiliwa Chama kilichosajiliwa kinapaswa kuwasilisha kwa Msajili kila ifikapo tarehe 31 Machi ya kila mwaka taarifa zifuatazo:(a) Taarifa za Fedha zilizokaguliwa kwa kipindi cha fedha kinachoishia tarehe 31 Desemba ya mwaka uliopita (b) Orodha ya Wanachama inayoonyesha jumla ya Wanachama kwa kipindi kinachoishia tarehe 31 Desemba ya mwaka uliopita (c) Majina ya viongozi walioteuliwa au kuchaguliwa na anuani zao ndani ya siku 30 tangu uteuzi au uchaguzi kufanyika (d) Mabadiliko ya kanuni ndani ya siku 30 kuanzia siku ya mabadiliko hayo Chama kina jukumu la kutunza kwa miaka iliyopungua mitano kumbukumbu zifuatazo:(a) Orodha ya Wanachama katika fomu maalum (b) Mihutasari ya vikao (c) Karatasi za kura 37 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Wajibu wa kuzingatia katiba ya chama Chama cha Wafanyakazi kinapaswa wakati wote kutekeleza shughuli zake kwa mujibu wa Katiba, kanuni na mazoea. Endapo itatokea Chama kimeshindwa kuzingatia Katiba yake, Msajili au Wanachama wanaweza kupeleka maombi Mahakama ya Kazi kutengua suala hilo lililofanyika kinyume cha Katiba. Kabla ya maombi kupelekwa Mahakamani, taratibu za ndani za Chama ni lazima zifuatwe kwanza isipokuwa kama kwa maslahi ya Chama ni vizuri maombi hayo kusikilizwa bila utaratibu wa ndani ya Chama.. Haki za Chama Chama cha Wafanyakazi kilichosajiliwa kinazo haki zifuatazo:(a) Haki ya kuingia eneo la Mwajiri (b) Makato ya ada (c) Kuwa na wawakilishi wake mahali pa kazi (d) Likizo kwa viongozi wake. Haki ya kuingia eleo la mwajiri Mwakilishi yeyote wa Chama cha Wafanyakazi kilichosajiliwa anayo haki ya kuingia eneo la Mwajiri kwa ajili ya:(a) Kuingiza Wanachama (b) Kuwasiliana na Wanachama (c) Kuwawakilisha Wanachama dhidi ya Mwajiri (d) Kuitisha mikutano ya Wafanyakazi (e) Kusimamia upigaji wa kura kwa mujibu wa Katiba ya Chama Hali kadhalika Chama kinayo haki ya kuanzisha Tawi lake mahali pa kazi ambapo kina Wanachama zaidi ya kumi. Chama cha Wafanyakazi kinachotambuliwa kinayo haki ya kupatiwa nyenzo na mwajiri kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake mahali pa kazi. 38 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Haki hii ya kuingia eneo la Mwajiri itatolewa kwa masharti maalumu kuhusiana na muda au mahali ambapo haki hizo zitatekelezwa kwa madhumuni ya kulinda maisha au mali au kuvurugika kwa kazi. Makato ya Ada Mwajiri anapaswa kukata ada ya Chama kutoka katika mshahara wa mfanyakazi endapo mfanyakazi huyo atatoa idhini ya kukatwa mshahara kwa kujaza Fomu Na. TUF 6. Mwajiri akishakata ada, anapaswa kuwasilisha ada hiyo kwa Chama ndani ya siku saba baada ya mwisho wa mwezi ambao makato haya yamefanyika. Mwajiri akishindwa kuwasilisha makato hayo ndani ya siku zilizotajwa hapo juu bila sababu za msingi anapaswa kukilipa Chama riba ya asilimia tano ya kiasi ambacho hakijawasilishwa kwa kila siku aliyokaa na fedha hizo. Mfanyakazi anaweza kutengua idhini yake ya kukatwa ada kwa kutoa taarifa ya mwezi mmoja kwa Mwajiri na Chama na mwezi mmoja ukipita mwajiri atasitisha makato hayo. Mwajiri anapowasilisha makato hayo kwa Chama anapaswa kuambatanisha orodha ya Wanachama waliokatwa ada na nakala ya kutengua idhini ya kukatwa ada kama ipo. Wawakilishi wa Chama Wawakilishi wa Chama mahali pa kazi wanapatikana kwa mujibu wa Katiba ya Chama aidha muda wao wa kushika madaraka au utaratibu wa kuwaondoa ni kwa mujibu wa Katiba ya Chama chenyewe. Chama cha Wafanyakazi kinayo haki ya kuwa na wawakilishi wake mahali pa kazi kwa kuzingatia idadi ya wanachama kama ifuatavyo (a) Wanachama wasiozidi tisa- Mwakilishi mmoja (b) Wanachama kuanzia kumi mpaka ishirini- wawakilishi watatu (c) Wanachama kuanzia ishirini na moja mpaka mia moja- wawakilishi kumi 39 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (d) Wanachama zaidi ya mia moja- wawakilishi kumi na tano, miongoni mwao watano lazima wawe wanawake kama wapo na ni wanachama. Wawakilishi wa Chama mahali pa kazi wana majukumu yafuatayo:(a) Kuwawakilisha Wanachama kwenye vikao vya kushughulikia malalamiko na nidhamu (b) Kuwasilisha hoja kwa niaba ya Wanachama kuhusiana na Kanuni; Afya na usalama na Ustawi wao. (c) Kushauriana na Mwajiri kuhusu tija mahali pa kazi (d) Kukiwakilisha Chama wakati wa ukaguzi na uchunguzi unaofanywa na wakaguzi kwa mujibu wa Sheria yoyote ya kazi. (e) Kuhakikisha Mwajiri anazingatia Sheria za kazi. (f) Kufanya kazi za Chama kwa mujibu wa Katiba ya Chama (g) Kuendeleza uhusiano mzuri kazini (h) Kutekeleza jukumu lolote walilokubaliana na Mwajiri. Wawakilishi wa Chama wanayo haki ya kupewa muda wa kutosha kutekeleza majukumu yao bila kukatwa mshahara na wanayo haki pia ya kupewa na mwajiri taarifa zote muhimu zitikazowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu. Haki hizi zitatolewa kwa masharti yatakayohakikisha haki hizi zinatekelezwa vizuri bila kuvuruga kazi. Likizo Wawakilishi wa Chama mahali pa kazi wanayo haki ya kupewa likizo ya malipo na Mwajiri kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo yanayohusiana na majukumu yao. Halikadhalika viongozi wa Chama cha Wafanyakazi na wa Shirikisho ambalo Chama ni mwanachama wanayo haki ya kupata likizo ya malipo kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya Chama au Shirikisho. 40 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Utaratibu wa kupata haki za chama Chama cha Wafanyakazi kilichosajiliwa kinachotaka kutekeleza haki za Chama kinapaswa kimtaarifu Mwajiri kwa kujaza Fomu na. CMA 3 kikiainisha haki ambazo kinataka kuzitekeleza na mahali pa kazi ambapo kinataka kikatekeleze haki hizo. Mwajiri akishapokea fomu hiyo anapaswa kukutana na Chama ndani ya siku thelathini na kama itawezekana kufikia makubaliano ya pamoja yatakayotoa haki hizo, na kuweka utaratibu wa kuzitekeleza. Endapo hapatakuwapo makubaliano au Mwajiri kushindwa kukutana na Chama ndani ya muda uliowekwa, Chama kinaweza kupeleka mgogoro huo mbele ya Tume kwa ajili ya usuluhishi. Usuluhishi ukishindikana Chama kinaweza kupeleka mgogoro huo Mahakama ya kazi kwa uamuzi. Usitishaji wa haki za chama Haki za Chama zinaweza kusitishwa iwapo Chama kitakiuka makubaliano ya msingi ya utoaji haki hizo au amri ya Mahakama inayotoa haki hizo. Ikitokea hali hiyo ya ukiukwaji wa makubaliano Mwajiri anaweza kupeleka mgogoro huo mbele ya Tume kwa ajili ya usuluhishi. Usuluhishi ukishindikana, anaweza kupeleka mgogoro huo Mahakama ya Kazi, akiiomba Mahakama isitishe makubaliano ya kutoa haki hizo au iondoe amri yake ya kutoa haki hizo. 41 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania SURA YA SABA MAJADILIANO YA PAMOJA Majadiliano ya pamoja ni majadiliano yanayofanyika baina ya Chama cha Wafanyakazi kinachotambuliwa na Mwajiri kama wakala wa Wafanyakazi katika majadiliano kwa upande mmoja, na Mwajiri au Jumuiya ya Waajiri kwa upande mwingine. Vyama vya Wafanyakazi zaidi ya kimoja vilivyosajiliwa vinaweza kuunda mseto na kutambuliwa kwa pamoja kama wakala wa wafanyakazi katika majadiliano ya pamoja. Majadiliano ya pamoja ni njia mojawapo ya kutatua migogoro ya kazi. Majadiliano haya yanaweza kuihusu sehemu moja ya kazi, au sehemu nyingi za kazi kwa pamoja. Utambuzi Ili Chama cha Wafanyakazi kiweze kushiriki katika majadiliano ya pamoja, kinapaswa kuingia katika makubaliano ya kutambuliwa na Mwajiri kama wakala pekee wa Wafanyakazi katika majadiliano ya pamoja. Sifa ya msingi kwa Chama kuweza kutambuliwa ni kuwa na Wanachama wengi miongoni mwa Wafanyakazi katika kitengo cha majadiliano. Kitengo cha majadiliano ni kundi la Wafanyakazi ambalo Chama kinatambuliwa au kinastahili kutambuliwa kama wakala wa kundi hilo la Wafanyakazi. Kwa lugha nyingine ni kundi ambalo litahusika na makubaliano yoyote yatokayofikiwa baina ya Chama na Mwajiri baada ya majadiliano. Kitengo cha majadiliano kinaweza kujumuisha kada maalum ya Wafanyakazi ambao wana maslahi yanayofanana. Utaratibu wa Chama kuomba kutambuliwa Chama cha Wafanyakazi kinachotaka kutambuliwa na Mwajiri kama wakala pekee wa wafanyakazi katika majadiliano ya pamoja, kinapaswa kujaza fomu maalum(Fomu Na. CMA 2), na kuwasilisha kwa mwajiri husika au Jumuiya ya Waajiri kutegemea wanataka kujadiliana na nani. Katika fomu hiyo, Chama 42 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania cha Wafanyakazi kinapaswa kupendekeza kitengo cha majadiliano wanachotaka kukiwakilisha na kuambatanisha ushahidi wa nyaraka unaothibitisha kuwa kina uwakilishi mkubwa katika kitengo hicho cha majadiliano. Mwajiri akishapokea fomu hiyo anapaswa kukutana na Chama cha Wafanyakazi husika ndani ya siku thelathini(30) na ikiwezekana wafikie makubaliano ya kukitambua Chama kama wakala pekee wa Wafanyakazi katika kitengo cha majadiliano. Endapo Mwajiri atashindwa kukutana na Chama cha Wafanyakazi ndani ya siku thelathini au Mwajiri na Chama wameshindwa kufikia makubaliano, Chama kinaweza kupeleka mgogoro huo mbele ya Tume kwa ajili ya usuluhishi. Usuluhishi utafanyika ndani ya siku thelathini kuanzia siku rufaa ilipopokelewa na Tume au zaidi ya siku thelathini kwa makubaliano ya maandishi ya pande husika. Ikitokea usuluhishi umeshindikana Chama kinaweza kupeleka mgogoro huo Mahakama ya Kazi kwa uamuzi. Mahakama ya Kazi inaweza kuiagiza Tume isimamie zoezi la upigaji kura iwapo mgogoro unahusu uwakilishi au idadi ya Wanachama katika kitengo cha majadiliano. Jukumu la kujadiliana kwa nia njema Mwajiri au Jumuiya ya Waajiri iliyokitambua Chama cha Wafanyakazi wanapaswa kujadiliana nacho kwa nia njema. Hali kadhilika Chama cha Wafanyakazi nacho, kina jukumu hilo hilo la kujadiliana kwa nia njema na Mwajiri au Jumuiya ya Waajiri iliyowatambua. Jukumu la kujadiliana kwa nia njema linajumuisha mambo yafuatayo:(a) Kuheshimu Wawakilishi wa pande zote (b) Kujiandaa kikamilifu na majadiliano kabla ya majadiliano yenyewe kwa kuandaa mapendekezo na kupata ridhaa ya wanaowawakilisha. (c) Kutobadilisha badilisha wawakilishi katika majadiliano bila sababu za msingi 43 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (d) Kuhudhuria vikao kwa wakati (e) Kutoa sababu kwa kila pendekezo lililowasilishwa. (f) Kupokea mapendekezo ya upande wa pili na kuyatafakari, na kama hayakubaliki, kutoa sababu za kutoyakubali. Jukumu la kujadiliana kwa nia njema linakitaka Chama kilichotambuliwa kuwawakilisha kwa haki Wafanyakazi wote bila kubagua ndani ya kitengo cha majadiliano, hata wasio Wanachama wake. Kinyume cha kujadiliana kwa nia njema ni kujadiliana kwa nia mbaya na hii hutokea pale ambapo vitendo vya upande husika vinaashiria hana nia ya kweli ya kufikia makubaliano. Vitendo ambavyo vinaweza kuchukuliwa kuwa ni kujadiliana kwa nia mbaya ni pamoja na:(a) Kutoa madai makubwa yasiyotekelezeka bila sababu za msingi (b) Kukataa bila sababu za msingi kupunguza baadhi ya mapendekezo (c) Kukataa kutoa taarifa zinazohitajika kuwezesha majadiliano kufanyika (d) Kutumia lugha isiyofaa, matusi, kejeli na dharau wakati wa majadiliano (e) Kuchelewesha majadiliano bila sababu za msingi (f) Kuweka masharti yasiyo na msingi ili majadiliano yaendelee (g) Kuwazunguka wawakilishi wa upande mwingine wakati wa mchakato wa majadiliano (h) Kuanza kuchukua hatua za upande mmoja kama vile kubadilisha masharti ya kazi au kugoma kabla majadiliano hayajamalizika. Mchakato wa majadiliano utakuwa umekamilika iwapo pande zote zitakuwa zimekubaliana au upande mmoja umetangaza kukwama kwa majadiliano. Upande wowote katika mchakato wa majadiliano unaweza kutangaza kukwama kwa majadiliano baada ya:(a) Upande huo kujaribu kwa nia njema kufikia makubaliano bila mafanikio baada ya kusubiri kwa kipindi kirefu. 44 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (b) Upande mwingine kutenda vitendo ambavyo vinaashiria hawataki kujadiliana (c) Upande mwingine unajadili kwa nia mbaya. Masuala yanayoweza kujadiliwa katika majadiliano ya pamoja Masuala yanayoweza kujadiliwa katika majadiliano ya pamoja ni kama yafuatayo:(a) Mishahara na aina nyingine za ujira (b) Masharti na hali ya ajira (i) Masharti ya ajira ni masharti yaliyomo katika mkataba wa ajira kwa kuelezwa waziwazi au kwa kuchukuliwa kuwa ni masharti ya ajira kama vile saa za kazi, muda wa likizo, muda wa notisi n.k. na (ii) Hali ya ajira ni mambo ambayo kwa kawaida yanaambatana na ajira kama vile Kanuni za kusimamia nidhamu mahali pa kazi, huduma za kantini, Afya na Usalama n.k. (c) Posho, marupurupu na mafao ya ajira (d) Sera na mazoea ya ajira kuhusiana na ajira mpya, uteuzi, mafunzo, uhamisho, upandaji vyeo, kusimamisha wafanyakazi, nidhamu na usitishaji wa ajira. (e) Uhusiano kazini ikiwemo:(i) Haki za Chama (ii) Taratibu za majadiliano na utatuzi wa migogoro (iii) Taratibu za malalamiko, nidhamu na usitishaji ajira. (f) Mambo yoyote yatakayokubaliwa na pande zote husika. 45 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Jukumu la kutoa taarifa muhimu Mwajiri analo jukumu la kutoa kwa Chama kinachotambulika, taarifa zote muhimu zitakazokisaidia Chama kushiriki kikamilifu, kwenye mashauriano na majadiliano ya pamoja na Mwajiri au Jumuiya ya Waajiri. Madhumuni ya kutoa taarifa hizo ni kuwezesha mchakato wa majadiliano au mashauriano uweze kufanyika kwa urahisi kadiri iwezekanavyo. Kuhakikisha majadiliano yanafanyika kwa nia njema, na kufanya mazingira ya kuaminiana kwa pande zote za majadiliano. Kwa kawaida Mwajiri anapaswa kutoa taarifa zile tu zinazohusiana na suala linalojadiliwa. Hata hivyo Mwajiri halazimishwi kutoa taarifa ambazo:(a) Anayo kinga kisheria kutozitoa (b) Akizitoa atakuwa anakiuka amri/zuio alilowekewa na Sheria au Mahakama (c) Ni za Siri, ambazo zinaweza kusababisha madhara kwa mfanyakazi au mwajiri iwapo zitatolewa, madhara kama Mwajiri kupoteza wateja, wagavi kukataa kumletea mali muhimu au huduma, mabenki kukataa kumkopesha, kushindwa kupata fedha za kuongeza mtaji wa biashara. (d) Taarifa binafsi za mfanyakazi bila ridhaa ya mfanyakazi husika. Utaratibu wa kuomba taarifa Kwa kawaida Chama cha Wafanyakazi kinapohitaji taarifa kinapaswa kumtaarifu Mwajiri kwa maandishi mapema iwezekanavyo, ili kutoa nafasi kwa mwajiri kuandaa na kuwasilisha taarifa hizo, hivyo Chama kinapaswa kieleze kwa ufasaha na usahihi ni taarifa zipi kinahitaji na sababu za kuhitaji taarifa hizo. Chama cha Wafanyakazi kitakachopewa taarifa za siri au za mtu binafsi kina wajibu wa kutunza siri hizo na kutozitoa taarifa hizo kwa mtu yeyote asiyehusika zaidi ya Wanachama na washauri wake. 46 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Makubaliano ya Pamoja Makubaliano ya pamoja ni makubaliano ya maandishi baina ya Chama cha Wafanyakazi kwa upande mmoja na Mwajiri au Jumuiya ya Waajiri kwa upande mwingine, kuhusiana na suala lolote la kazi. Makubaliano haya yanapaswa kusainiwa na pande zote husika na yakishatiwa sahihi yanazibana pande zote kuyatekeleza isipokuwa kama itakubaliwa vinginevyo. Licha ya kuzibana pande husika za makubaliano hayo yaani Chama cha Wafanyakazi na Mwajiri au Jumuiya ya Waajiri, makubaliano hayo yanawabana pia Wanachama wa Chama husika na Wafanyakazi ambao sio Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi kilichoingia katika makubaliano waliomo katika kitengo cha majadiliano. Makubaliano hayo yataendelea kuwabana Waajiri au Wafanyakazi waliokuwa sehemu ya makubaliano hayo wakati yanaanza kutumika wakiwemo Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi au Jumuiya ya Waajiri waliojiuzulu. Makubaliano hayo yatawabana pia Waajiri na wafanyakazi waliojiunga na Jumuiya ya Waajiri au Chama cha Wafanyakazi baada ya makubaliano hayo kuanza kutumika. Makubaliano hayo yanaweza kusitishwa na upande wowote kwa kutoa notisi isipokuwa kama itakubaliwa vinginevyo. Nakala ya makubaliano hayo inapaswa ipelekwe kwa Kamishna wa Kazi. Makubaliano ya ada ya uwakala Makubaliano ya ada ya uwakala ni makubaliano yanayofikiwa baina ya Chama cha Wafanyakazi kinachotambuliwa kwa upande mmoja, na Mwajiri kwa upande mwingine, kukata ada ya uwakala kutoka katika mishahara ya Wafanyakazi wasio wanachama kwa sababu ya kufaidika na huduma ya Chama, ili mradi makubaliano hayo yazingatie mambo yafuatayo:(a) Wafanyakazi watakaohusika ni wale waliomo kwenye kitengo cha majadiliano peke yake. 47 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (b) Wafanyakazi wasio Wanachama wasilazimishwe kwa namna yoyote kuwa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi. (c) Kiwango cha ada ya uwakala isizidi kiwango cha ada wanayolipa Wanachama (d) Ada ya uwakala itakayokatwa kutoka kwa wasiowanachama itunzwe na Chama katika akaunti tofauti na akaunti ya ada za Wanachama (e) Pesa zitakazokusanywa zitumike katika kuendeleza na kulinda maslahi ya kijamii na kiuchumi ya Wafanyakazi katika sehemu hiyo ya kazi. Maslahi ya kijamii na kiuchumi ya Wafanyakazi ni kama yafuatayo:Masuala ya kazi yanayoathiri ajira au uhusiano kazini, elimu ya wafanyakazi n.k. Ushirikishwaji wafanyakazi Chama cha Wafanyakazi kinachotambuliwa kwa upande mmoja na Mwajiri au Jumuiya ya Waajiri, wanaweza kufikia makubaliano ya pamoja ya kuanzisha Baraza la ushirikishwaji Wafanyakazi mahali pa kazi na katika kufanya hivyo wanaweza kuomba msaada na ushauri wa Tume. Kuondolewa kwa utambuzi Utambuzi wa Chama cha Wafanyakazi kama wakala pekee wa Wafanyakazi katika kitengo cha majadiliano unaweza kuondolewa iwapo wanachama wa Chama hicho watapungua na kuwa pungufu ya nusu ya Wafanyakazi katika kitengo cha majadiliano. Ili mradi iwe imepita miezi sita(6) kuanzia tarehe ya Chama kutambuliwa. Utaratibu wa kuondoa utambuzi Chama kikipoteza uwakilishi katika kitengo cha majadiliano, Mwajiri anapaswa kukipa notisi ya miezi mitatu(3) kiongeze uwakilishi wake. Iwapo Chama kitashindwa kuongeza idadi ya Wanachama baada ya miezi hiyo mitatu kupita, Mwajiri anayo haki ya kuondoa utambuzi. Chama kinachotambuliwa kikipoteza uwakilishi, Chama kingine ambacho kina uwakilishi mkubwa kinaweza kuomba kutambuliwa kama wakala pekee wa majadiliano wa Wafanyakazi katika kitengo cha majadiliano. 48 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania SURA YA NANE MIGOMO Mgomo ni usimamishaji wa kazi, unaofanywa na Wafanyakazi kwa lengo la kumlazimisha au kumshurutisha Mwajiri wao au Mwajiri mwingine au Jumuiya ya Waajiri ambayo Mwajiri wao ni mwanachama, kukubali madai ya Wafanyakazi, au Mwajiri kubadili au kuacha madai yake dhidi ya Wafanyakazi, madai ambayo yanahusiana na mgogoro wa maslahi. Haki ya kugoma Kila mfanyakazi anayo haki ya kugoma. Hata hivyo haki hii ya kugoma ni kwa migogoro ya maslahi peke yake. Kwa msingi huo chini ya Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini, Wafanyakazi hawaruhusiwi kugoma iwapo mgogoro wao ni lalamiko au mgogoro wa kudai haki. Kuzuizi cha kugoma Pamoja na haki ya kugoma kutolewa kwa kila mfanyakazi, wapo baadhi ya Wafanyakazi ambao wamenyimwa haki hiyo. Wafanyakazi hao ni hawa wafuatao:(i) Wafanyakazi katika huduma muhimu (ii) Wafanyakazi ambao wanapaswa kuendelea na kazi wakati wa mgomo kwa makubaliano ya pamoja ya utoaji huduma kwa kiwango cha chini. (iii) Wafanyakazi ambao wanabanwa na makubaliano ya kupeleka mgogoro huo kwenye uamuzi (iv) Wafanyakazi ambao wanabanwa na makubaliano ya pamoja au TUZO ya mwamuzi inayosimamia suala la mgogoro. (v) Mahakimu, Waendesha Mashitaka au Watumishi wengine wa Mahakama. (vi) Wafanyakazi wanaobanwa na Tangazo la Kima cha Chini cha Mshahara na Masharti ya kazi yanayosimamia suala la mgogoro katika mwaka wa kwanza wa kutumika Tangazo hilo. 49 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Utaratibu wa mgomo Ili mgomo uwe halali ni lazima wafanyakazi wafuate hatua zifuatazo:(a) Mgogoro uwe mgogoro wa maslahi (b) Mgogoro uwasilishwe Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kwa ajili ya usuluhishi kwa kutumia fomu maalum(Fomu CMA 1) (c) Mgogoro uwe umeshindikana kusuluhishwa ndani ya siku 30 au zaidi kadri pande husika zitakavyokubaliana (d) Kura za kuunga mkono mgomo zipigwe na wafanyakazi husika kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Wafanyakazi. (e) Notisi ya saa 48 ya kuanza mgomo itolewe kwa Mwajiri. Saa 48 zitakazohesabiwa ni saa za kawaida za kazi na notisi ni lazima ieleze mgomo utakuwa wa siku ngapi. Hata hivyo wafanyakazi wanaweza kugoma bila kufuata utaratibu huo hapo juu, endapo itatokea Mwajiri akabadilisha masharti ya kazi bila kushauriana nao. Endapo itatokea hali hiyo, wafanyakazi wanachotakiwa kufanya ni kuwasillisha mgogoro kwenye Tume kwa fomu maalum(Fomu CMA 1) wakimtaka Mwajiri kutotekeleza mabadiliko hayo au kama ameshaanza kutekeleza, kuyarejesha masharti ya awali kabla ya mabadiliko. Endapo Mwajiri hatatekeleza madai yaliyoelezwa na Wafanyakazi ndani ya saa 48 kuanzia saa aliyopokea nakala ya fomu ya mgogoro, wafanyakazi wanaweza kugoma. Vitendo vinavyokatazwa wakati wa mgomo (a) Piketi, kuunga mkono mgomo (b) Kutoajiri na kutumia wafanyakazi wapya mbadala wakati wa mgomo (c) Kuwafungia Waajiri ndani ya eneo la kazi (d) Kuwazuia Waajiri kuingia katika eneo la kazi 50 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Kiwango cha chini cha utoaji huduma Chama cha Wafanyakazi na mwajiri wanaweza kufikia makubaliano ya pamoja ya utoaji wa huduma kwa kiwango cha chini wakati wa mgomo ambapo Wafanyakazi wachache wataendelea kutoa huduma wakati mgomo ukiendelea. Endapo hakuna makubaliano ya pamoja, Mwajiri anaweza kuwasilisha maombi kwenye kamati ya Huduma Muhimu, kubainisha au kuomba baadhi ya wafanyakazi waendelee na kazi wakati wa mgomo iwapo kiwango hicho cha chini cha huduma ni muhimu katika kuzuia uharibifu wa mali au mashine wakati wa mgomo. Madhara ya mgomo usiofuata utaratibu au kutenda vitendo vinavyokatazwa Endapo wafanyakazi wanashiriki mgomo ambao unafanyika bila kuzingatia utaratibu uliowekwa na Sheria, au wanatenda vitendo vilivyokatazwa, Mahakama ya Kazi imepewa mamlaka ya: (a) Kutoa Amri ya Zuio kumzuia mtu yeyote kushiriki katika mgomo huo au kutenda kitendo kilichokatazwa. (b) Kuamuru kulipwa fidia kwa hasara iliyosababishwa na mgomo huo au kitendo hicho kilichokatazwa. Kitendo cha kupinga Kitendo cha kupinga ni usimamishaji wa kazi unaofanywa na Wafanyakazi kwa madhumuni ya kukuza na kulinda maslahi yao ya kijamii na kiuchumi, lakini sio kwa madhumuni ya kugoma au kwa haki ambayo Sheria imeweka utaratibu wa kuidai. Utaratibu wa kushiriki katika kitendo cha kupinga. Mfanyakazi anaweza kushiriki katika kitendo cha kupinga iwapo:(a) Kitendo hicho kimeitishwa na Chama cha Wafanyakazi au Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi. (b) Chama au Shirikisho liwe limetoa notisi kwa Baraza ikieleza:(i) Sababu za kitendo hicho, na (ii) Muda na namna kitendo hicho kitafanyika. 51 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (c) Siku thelathini ziwe zimepita kuanzia tarehe ya notisi kupokelewa kwenye Baraza. (d) Chama au Shirikisho liwe limetoa notisi ya angalau siku kumi na nne (14) ya kuanza kwa kitendo cha kupinga. Kizuizi cha kushiriki kitendo cha kupinga. Wafanyakazi katika huduma muhimu na wale iliyokubaliwa watoe kiwango cha chini cha huduma, hawaruhisiwi kushiriki katika kitengo cha kupinga. 52 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania SURA YA TISA UTATUZI WA MIGOGORO Migogoro ya kazi ni migogoro inayohusisha Mwajiri au Jumuiya ya Waajiri kwa upande mmoja na mfanyakazi au Chama cha Wafanyakazi kwa upande mwingine. Migogoro ya kazi imegawanyika katika sehemu kuu mbili, migogoro ya maslahi na migogoro ya kudai haki au lalamiko. Mgogoro wa maslahi Mgogoro wa maslahi ni mgogoro wowote ambao si lalamiko. Kwa mfano:(a) Mgogoro kuhusu nyongeza ya mshahara (b) Mgogoro wa kuhusu kupunguzwa au kuongezwa saa za kazi (c) Mgogoro kuhusu kurejewa makubaliano ya pamoja n.k. Lalamiko Lalalamiko ni mgogoro wowote unaotokana na matumizi, tafsiri na utekelezaji wa:(a) Makubaliano au mkataba baina ya Mwajiri na Mfanyakazi (b) Makubaliano ya pamoja baina ya Chama cha Wafanyakazi na Mwajiri au Jumuiya ya Waajiri. (c) Sheria za Kazi (d) Sehemu VII ya Sheria ya Merchant Shipping Act, 2003 Mfano wa mgogoro wa haki au lalamiko ni:(a) Kushindwa kulipa mshahara (b) Kukiuka makubaliano ya pamoja (c) Kushindwa au kukataa kutekeleza yaliyokubaliwa katika Mkataba wa Ajira (d) Kukiuka Sheria 53 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Taratibu za utatuzi wa migogoro ya kazi Sheria imeweka utaratibu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya Usuluhishi, Uamuzi na Mahakama. Vile vile Sheria imetoa nafasi kwa wadau kukubaliana njia au namna ya kutatua migogoro yao. Migogoro yote ya kazi ukiachia ile ambayo wadau wamekubaliana vinginevyo inapaswa ianzie hatua ya usuluhishi kwenye Tume isipokuwa pale ambapo Sheria imeelekeza vinginevyo. Usuluhishi Usuluhishi ni hatua ya kwanza kabisa ya utatuzi wa migogoro. Uwasilishaji mgogoro mbele ya Tum e Mgogoro utawasilishwa kwenye Tume kwa kutumia fomu maalum ya rufaa. (Fomu CMA 1) na utawasilishwa katika Ofisi ya Tume inayosimamia eneo ambamo mgogoro umetokea. Kabla ya kuiwasilisha kwenye Tume, mlalamikaji anapaswa ampatie nakala ya fomu hiyo mlalamikiwa na anapoiwasilisha kwenye Tume anatakiwa kutoa ushahidi unaothibitisha kuwa tayari alishampelekea nakala ya fomu hiyo mlalamikiwa. Fomu hiyo inaweza kupelekwa kwa mlalamikiwa kwa njia kuu tatu:- Mkono - Nukushi - Rejista ya posta Muda wa kuwasilisha mgogoro kwenye Tume Migogoro yote inayohusu usitishaji ajira inapaswa iwasilishwe kwenye Tume ndani ya siku thelathini(30) kuanzia siku ulipotokea, na migogoro mingine inapawa iwasilishwe ndani ya siku sitini(60). Endapo mgogoro utachelewa kuwasilishwa ndani ya siku zinazotakiwa, mlalamikaji anapaswa kujaza fomu maalum(fomu CMA 7) ya kuomba kuleta mgogoro wake nje ya muda. Fomu hiyo inapaswa iambatane na Taarifa ya maombi pamoja na hati ya kiapo. Kuteuliwa msuluhishi Mara baada ya kupokea rufaa iliyowasilishwa Tume itateua Msuluhishi wa kusuluhisha mgogoro huo na itatoa notisi(hati wito) ya angalau siku kumi na nne(14) kwa wadaawa. 54 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Usuluhishi ni nini? Usuluhishi ni mchakato, katika mchakato huo mtu huru asiyekuwa na upande wowote katika mgogoro husika anajaribu kuwasaidia wadaawa kutatua mgogoro. Katika mchakato huo Msuluhishi anaweza kukutana na wadaawa kwa pamoja au mmoja mmoja pekee. Msuluhishi hapaswi kulazimisha watu wapatane, anachoweza kufanya ni kutoa mapendekezo yatakayosaidia kumaliza mgogoro. Wenye dhima ya kumaliza mgogoro ni wadaawa wenyewe. Msuluhishi anazo siku thelathini(30) za kusuluhisha, siku hizo zinaweza kuongezwa kwa makubaliano ya maandishi ya wadaawa wenyewe. Mara baada ya usuluhishi kufikia tamati, Msuluhishi anapaswa kutoa hati ya kusuluhisha au kutosuluhisha Mgogoro(Fomu CMA 5) akiainisha aina ya mgogoro na kueleza iwapo mgogoro umesuluhishwa au hapana. Endapo mgogoro umesuluhishwa, Msuluhishi anapaswa kuandika makubaliano hayo vizuri ambayo yatasainiwa na pande zote husika. Upande wowote unaweza kuomba makubaliano hayo yawe TUZO ya Mwamuzi. Uwakilishi wakati wa usuluhishi Mdaawa katika mgogoro wakati wa usuluhishi anaweza kuwakilishwa na:(a) Ofisa wa Chama cha Wafanyakazi au mwanachama mwenzake. (b) Wakili (c) Mtu yeyote aliyemchagua Hatua zinazofuata usuluhishi ukishindikana Endapo msuluhishi atashindwa kusuluhisha, mdaawa anaweza:(a) Iwapo mgogoro ni wa maslahi (i) Kutoa notisi ya nia ya kugoma au kufungia nje (b) Iwapo mgogoro ni mgogoro wa haki au lalamiko:(i) Kupeleka mgogoro huo kwenye hatua ya uamuzi; au (ii) Kupeleka mgogoro huo Mahakama ya Kazi. 55 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Hata hivyo Sheria inampa msuluhishi uwezo na mamlaka ya kuendelea kusuluhisha mgogoro huo hata baada ya mgogoro kuingia hatua nyingine. Madhara ya kushindwa kuhudhuria Usuluhishi Madhara ya kutohudhuria usuluhishi yanategemea aina ya mgogoro. Iwapo mgogoro ni mgogoro wa maslahi na aliyeshindwa kuhudhuria usuluhishi ni mlalamikaji, Msuluhishi anaweza kuongeza siku thelathini(30) zaidi ya zile alizonazo kisheria. Na kama mlalamikiwa ndiye aliyeshindwa kuhudhuria, msuluhishi anaweza kupunguza siku za usuluhishi. Iwapo mgogoro ni mgogoro wa haki au lalamiko, msuluhishi anaweza kuutupilia mbali mgogoro huo, endapo aliyeshindwa kuhudhuria ni mlalamikaji au kusikiliza shauri upande mmoja endapo aliyeshindwa kuhudhuria ni mlalamikiwa. Kabla ya kuchukua hatua hiyo Tume itajiridhisha kuwa wadaawa walitaarifiwa ipasavyo. Hata hivyo Tume inaweza kubadilisha uamuzi wake endapo upande ulioumizwa na uamuzi huo, utawasilisha maombi kwa utaratibu uliowekwa mbele ya Tume, ndani ya siku kumi na nne(14) na tume kuridhika kuwa mdaawa alikuwa na sababu za msingi zilizomfanya ashindwe kuhudhuria. Uamuzi Uamuzi ni mchakato ambao mtu aliyeteuliwa kuwa Mwamuzi anasikiliza ushahidi na hoja za wadaawa na kisha kutatua mgogoro kwa kutoa uamuzi na TUZO ya maandishi, ikieleza sababu za uamuzi huo. Migogoro inayotatuliwa kwa njia ya uamuzi Kama ilivyo katika usuluhishi mgogoro katika hatua ya Uamuzi utasikilizwa na kuamuliwa katika Ofisi ya Tume inayosimamia eneo ambamo mgogoro umetokea. Migogoro ambayo itasikilizwa na kuamuliwa kwa njia ya uamuzi ni:(a) Migogoro ya maslahi katika huduma muhimu (b) Lalamiko juu ya (i) Uhalali wa kusitisha ajira (ii) Madai yoyote yatokanayo na ukiukwaji wa Mkataba wa ajira ambayo kiasi kinachodaiwa kipo ndani ya mamlaka ya kifedha ya Mahakama ya Hakimu Mkazi 56 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (iii) Mgogoro wowote utakaoletwa na Mahakama ya Kazi kwa ajili ya kuamuliwa na Tume Utaratibu wa kuwasilisha mgogoro kwa ajili ya uamuzi Mara baada ya Msuluhishi kushindwa kusuluhisha mgogoro, atatoa hati ya kushindwa kusuluhisha, akieleza waziwazi aina ya mgogoro pamoja na masuala yasiyobishaniwa na yanayobishaniwa. Hati ya kushindwa kusuluhisha itatolewa na msuluhishi, mlalamikaji anaweza kuomba Tume iupeleke mgogoro huo katika hatua ya uamuzi. Wadaawa wanaposhindwa kutatua mgogoro wao kwa njia ya usuluhishi na mgogoro kuwasilishwa katika ngazi ya uamuzu, Tume itateua Mwamuzi wa kusikiliza na kuamua mgogoro huo na itatoa notisi(hati wito) ya angalau siku kumi na nne(14) kwa wadaawa. Utaratibu wa kusikiliza na kuamua mgogoro Mwamuzi anayo mamlaka ya kuamua namna atakavyoliendesha shauri kwa madhumuni ya kutatua mgogoro husika kwa haraka na kwa haki na kwa kuzingatia kiini cha mgogoro bila kubanwa sana na masuala ya kiufundi. Katika ngazi ya uamuzi shauri litapitia hatua tano muhimu zifuatazo:(i) Utangulizi (ii) Hoja za ufunguzi na kuanisha masuala ya kubishaniwa (iii) Ushahidi (iv) Hoja za hitimisho; na (v) Tuzo Uwakilishi katika ngazi ya uamuzi Mdaawa katika mgogoro uliopo katika ngazi ya uamuzi anaweza kuwakilishwa na:(a) Ofisa wa Chama cha Wafanyakazi au mwanachama wenzake; (b) Wakili (c) Mtu yeyote aliyemchagua 57 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Madhara ya kushindwa kuhudhuria usikilizaji wa shauri Endapo upande wowote katika shauri utashindwa kuhudhuria usikilizaji wa shauri, mwamuzi anaweza kufanya mambo yafuatayo:(a) Iwapo aliyeshindwa kuhudhuria ni mlalamikaji, Mwamuzi anaweza kulifuta shauri. (b) Iwapo aliyeshindwa kuhudhuria shauri ni mlalamikiwa, Mwamuzi anaweza kusikiliza shauri upande mmoja. Mwamuzi anaweza kutengua uamuzi wake, endapo upande ulioumizwa na uamuzi huo utawasilisha maombi ndani ya siku kumi na nne(14), na Tume kuridhika kuwa mdaawa alikuwa na sababu za msingi zilizomfanya ashindwe kuhudhuria. Utoaji tuzo Mwamuzi akishamaliza kusikiliza shauri anapaswa kutoa uamuzi uliosainiwa pamoja na Tuzo ndani ya siku thelathini(30) akieleza sababu za uamuzi huo. Tuzo itakayotolewa itazibana pande zote za mgogoro na inaweza kukazwa katika Mahakama ya Kazi kama Amri ya Mahakama. Marejeo Hakuna haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi na Tuzo ya Mwamuzi. Mtu asiyeridhika na uamuzi na Tuzo ya Mwamuzi anaweza kuwasilisha maombi ya marejeo Mahakama ya Kazi ndani ya wiki sita(6) kuanzia tarehe ya uamuzi na Tuzo hiyo. Mahakama ya Kazi inaweza kutengua uamuzi na Tuzo ya Mwamuzi kwa maombi au kwa hatua zake yenyewe, endapo itabainika kulikuwepo kasoro za kisheria katika uamuzi na Tuzo hiyo. MAHAKAMA Mahakama ya Kazi inayo mamlaka ya kipekee kuhusiana na masuala ya matumizi, tafsiri na utekelezaji wa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini na Sheria nyingine za kazi pamoja na kutoa maamuzi juu ya:(a) Rufaa kutokana na maamuzi ya Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri. 58 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (b) Mapitio na marejeo ya:(i) Tuzo ya Mwamuzi (ii) Maamuzi ya Kamati ya Huduma Muhimu (c) Mapitio ya maamuzi, Kanuni na miongozo itolewayo na Waziri (d) Malalamiko yanayopaswa kusikilizwa na Mahakama ya Kazi (e) Migogoro inayopaswa kutolewa maamuzi na Mahakama ya Kazi (f) Maombi ikiwemo:(i) Amri ya tamko au (ii) Amri ya Zuio Utaratibu wa kuwasilisha Lalamiko Mlalamikaji yeyote anayetaka kuwasilisha lalamiko lake Mahakama ya Kazi atawasilisha lalamiko hilo kwa kuwasilisha maelezo ya lalamiko kama ilivyoelekezwa katika Fomu na. 1 ya jedwali la kanuni za Mahakama Kazi, 2007. Lalamiko linapaswa liwasilishwe Mahakamani ndani ya siku thelathini(30) tangu kushindwa usuluhishi mbele ya Tume, endapo lalamiko hilo linahusu usitishaji wa ajira na siku sitini(60) kwa aina nyingine ya malalamiko. Kesi ya Uwakilishi Endapo walalamikaji wengi wana malalamiko yanayofanana dhidi ya Mwajiri wanaweza kufungua shauri la uwakilishi kwa ruhusa ya Mahakama ambapo mmoja au wachache miongoni mwao watawawakilisha walalamikaji wengine. Uwasilishaji wa nyaraka Mahakamani Nyaraka zote zitawasilishwa kwa Msajili zikiwa katika nakala za kutosha kwa:(a) Mkono; au (b) Rejista ya posta; au (c) Kwa nukushi au barua pepe Nyaraka zitakazowasilishwa kwa mkono ni lazima ziwe nakala halisi na endapo nyaraka hizo zitawasilishwa kwa nukushi au barua pepe, nakala zake halisi ni lazima ziwasilishwe ndani ya siku kumi na tano kuanzia siku zilipotumwa. 59 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Kikao cha Awali na Usuluhishi Mara baada ya pande zote kuwasilisha nyaraka zao kwa maana ya maelezo ya lalamiko, mabezo na maelezo ya nyongeza ya lalamiko, Msajili ataitisha kikao cha awali na kujaribu kutatua mgogoro kwa njia ya usuluhishi pamoja na kujaribu kukubaliana juu ya mambo mbalimbali ya msingi. Endapo wadaawa watafikia makubaliano ya kumaliza mgogoro, Msajili atatayarisha hati ya makubaliano itakayosainiwa na pande zote za mgogoro na makubaliano hayo yatakuwa Tuzo au Amri ya Mahakama. Endapo Wadaawa watashindwa kumaliza mgogoro wao kwa njia ya usuluhishi, watatayarisha tamko la pamoja la kushindwa kutatua mgogoro na kutia sahihi zao. Baada ya hapo Msajili atawasilisha Jalada ya kesi hiyo kwa Mheshimiwa Jaji kwa maelekezo na hatua zaidi. Maombi Maombi ya mapitio, marejeo na yale ya kingwala yatawasilishwa kwa njia ya maombi au samansi ya faragha ikiungwa mkono na hati ya kiapo. Maombi mengine yatawasilishwa kwa njia ya taarifa ya maombi ikiungwa mkono na hati ya kiapo. Rufaa Rufaa itawasilishwa, kwanza kwa kutoa notisi ya rufaa kwa mtu au taasisi ambayo uamuzi wake unakatiwa rufaa na nakala kuwasilishwa kwa Msajili wa Mahakama. Mara baada ya kupokea notisi ya rufaa mtu au taasisi ambayo uamuzi wake unakatiwa rufaa, itatayarisha mwenendo wa shauri kwa maandishi na sababu za uamuzi na kuwasilisha kwa Msajili wa Mahakama ndani ya siku kumi na tano. Msajili akishapokea nyaraka hizo atamkabidhi mrufani ambaye anapaswa kutayarisha hoja za rufaa na kuziwasilisha mahakamani ndani ya siku kumi na tano tangu akabidhiwe nyaraka. Mrufani anapaswa kumpa mjibu rufani nakala ya hoja zake za rufaa. Utatuzi wa migogoro kwa makubaliano Wadau wanaweza kukubaliana kutatua migogoro yao kwa utaratibu wa uamuzi chini ya“The Arbitration Act” na kwa utaratibu wa Usuluhishi na uamuzi kwa mujibu wa makubaliano ya pamoja ili mradi migogoro hiyo itasuluhishwa na kuamuliwa, kitaalam haraka na kwa haki. 60 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania SURA YA KUMI SHERIA YA BARAZA LA MAJADILIANO LA UTUMISHI WA UMMA, 2003 (PUBLIC SERVICE/NEGOTIATING MACHINERY ACT 2003) Sheria hii lengo lake ni kuwezesha ushirikishwaji wa watumishi wa Umma katika majadiliano na Serikali kuhusu maslahi na ustawi wao na kutoa nafasi kwa watumishi wa umma kujadili na kuishauri Serikali masuala mbalimbali yahusuyo utumishi wa umma. Sheria pia imeweka utaratibu wa utatuzi wa migogoro katika utumishi wa umma. UANZISHWAJI WA MABARAZA YA PAMOJA Madhumuni ya kuanzishwa mabaraza ya pamoja ni:(a) Kujenga ushirikiano baina ya Serikali kama mwajiri na watumishi wa Umma kupitia vyama vyao vya Wafanyakazi. (b) Kuweka mazingira yatakayowezesha kufanyika kwa majadiliano baina ya Serikali na watumishi wa Umma kuhusu masuala yahusuyo ufanisi na ustawi wa watumishi wa umma na; (c) Kuweka mfumo wa kushughulikia Malalamiko ya watumishi wa umma. Mabaraza hayo ya pamoja ni haya yafuatayo:(a) Baraza la Pamoja Serikali Kuu. (b) Baraza la Pamoja la Walimu. (c) Baraza la Pamoja la Serikali za Mitaa. (d) Baraza la Pamoja la Afya. (e) Baraza la Pamoja Zimamoto, Uokoaji na Uhamiaji. Mabaraza haya ni vyombo vya majadiliano vinavyotoa uwanja kwa watumishi wa Umma kushirikishwa. Muundo wa Mabaraza haya ni kama ifuatavyo:(a) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wanaoteuliwa na Waziri anayehusika na utumishi wa Umma kutoka katika majina mawili yaliyopendekezwa na Chama cha Wafanyakazi na Waziri wa Wizara husika. 61 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (b) Watumishi wa umma wanne wanaoteuliwa na Chama cha Wafanyakazi na Katibu. (c) Maofisa wanne wa Serikali wanaoteuliwa na Waziri anayehusika na utumishi wa umma wakiwakilisha:(i) Wizara inayohusika na utumishi wa umma. (ii) Wizara inayohusika na Fedha. (iii) Wizara inayohusika na masuala ya uhusiano kazini. (iv) Wizara mama inayohusika na huduma ambamo limeundwa. Baraza Chama cha Wafanyakazi na Waziri wahakikishe wanateua watu ambao wana uwezo wa kufanya maamuzi wakati wa majadiliano. MUDA WA KUKAA MADARAKANI MWENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watakaa katika madaraka yao kwa kipindi cha miaka mitatu na wanaweza kuteuliwa kwa kipindi kingine kimoja. KAZI ZA BARAZA LA PAMOJA Kazi za Baraza Ni:(a) Kuishauri Serikali kuhusiana na masuala yanayohusu ustawi wa watumishi wa umma. (b) Kujadili na kutoa mapendekezo kwa Serikali kwa suala lolote linalohusu maslahi, ustawi na ufanisi kwa upande wa watumishi wa umma. (c) Kujadili na kutoa ushauri kwa Serikali kwenye jambo lolote ambalo Serikali imeomba ushauri. (d) Kujadili kuhusu masharti na matakwa ya ajira kwa watumishi wa umma. (e) Kujadili jambo lolote litakaloletwa na Baraza la Pamoja la utumishi wa umma. 62 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania AKIDI NA VIKAO Akidi inayotakiwa kwa ajili ya kikao kufanyika ni wajumbe saba(7). Baraza litafanya vikao viwili kwa mwaka ndani ya robo mwaka ya kwanza ya mwaka wa fedha wa Serikali. Baraza pia linaweza kuitisha vikao visivyo vya kawaida iwapo litatokea jambo linalohitaji kufanyiwa kazi na kuamuliwa. MAAMUZI YA MABARAZA YA PAMOJA Maamuzi yote yatakayofanywa na Baraza la Pamoja juu ya jambo lolote ni lazima yapelekwe kwenye Baraza la Pamoja la Utumishi wa Umma kwa kuidhinishwa. Baraza la Pamoja la Utumishi wa Umma likishapokea uamuzi wa Baraza la Pamoja kwa ajili ya kuidhinishwa linaweza kufanya mambo yafuatayo:(a) Kuidhinisha baada ya kufanya marekebisho au bila kufanya marekebisho na kupeleka uamuzi huo kwa Waziri, au; (b) Kuahirisha uidhinishaji mpaka hapo muda muafaka utakapowadia au; (c) Kurejesha tena jambo hilo kwa Baraza la Pamoja kwa maelekezo ya kuangaliwa upya jambo hilo. BARAZA KUU LA PAMOJA LA UTUMISHI WA UMMA Baraza hili ndilo chombo cha juu cha majadiliano na ushauri katika utumishi wa umma. Baraza hili linaundwa na wajumbe wafuatao: (a) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wanaoteuliwa na Rais kutoka katika orodha ya majina yanayowasilishwa na Waziri. (b) Wajumbe wanane kutoka Vyama vya Wafanyakazi wanaoteuliwa na vyama vya Wafanyakazi. (c) Wajumbe nane wanaoteuliwa na Waziri kuwakilisha Serikali. 63 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Mtu yeyote ambaye ni mwanachama wa Chama cha Wafanyakazi au mtumishi wa Umma hapaswi kuwa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti. Katibu wa Baraza atateuliwa na Waziri kutoka miongoni mwa watumishi wa umma na Katibu Msaidizi wa Baraza atateuliwa na Vyama vya Wafanyakazi. KAZI ZA BARAZA KUU LA PAMOJA LA UTUMISHI WA UMMA Kazi za Baraza Kuu la Pamoja la utumishi wa umma ni kama ifuatavyo:(a) Kuishauri Serikali juu ya mambo yanayohusu ustawi wa watumishi wa Umma; (b) Kujadili na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya jambo lolote kuhusu maslahi, ustawi na ufanisi kwa upande wa watumishi wa Umma; (c) Kujadili na kutoa ushauri kwa Serikali juu ya jambo lolote ambalo Serikali imeomba ushauri wa Baraza; (d) Kufanya majadiliano juu ya mambo mbalimbali kuhusu masharti na matakwa ya ajira kwa watumishi wa umma kwa ujumla au kwa kundi la watumishi wa umma; (e) Kuidhinisha na kusajili au kujadili jambo lililowasilishwa kutoka kwenye Mabaraza ya Pamoja; (f) Kuamua rufaa zilizowasilishwa dhidi ya maamuzi ya Mabaraza ya Pamoja; na; (g) Kuanzisha jambo lolote muhimu na kulipeleka kwenye Mabaraza ya Pamoja kwa ajili ya kujadiliwa na kuamuliwa. KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA Ni marufuku kwa Baraza Kuu la Pamoja la utumishi wa Umma kujadili, kutoa ushauri au mapendekezo kuhusiana na kima cha chini cha mshahara au jambo lolote linalohusiana na Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara au Baraza la Ujira au chombo chochote kilichoteuliwa kufanya shughuli hiyo kwa mujibu wa sheria inayohusika na masuala ya kima cha chini cha mshahara. 64 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Iwapo litajitokeza suala lolote kuhusiana na kima cha chini cha mshahara au jambo lolote linalohusiana na Bodi ya Ujira au Baraza la Ujira au chombo chochote kilichoteuliwa kufanya shughuli hiyo, basi jambo hilo linapaswa kupelekekwa kwenye chombo husika. MUDA WA KUKAA MADARAKANI Mjumbe wa Baraza Kuu la Pamoja la Utumishi wa Umma atakaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu(3) na anaweza kuteuliwa tena. AKIDI NA VIKAO Akidi ya kikao ni wajumbe kumi na nne(14). Baraza litafanya kikao cha kawaida mara moja katika kila mwaka na litajitengenezea taratibu zake lenyewe za kuendesha vikao vyake. Baraza linapaswa kufanya kikao chake cha kawaida katika robo mwaka ya pili ya mwaka wa fedha wa Serikali na linaweza kufanya kikao kisicho cha kawaida wakati wowote litakapojitokeza jambo linalolazimu kikao kuitishwa au mara baada ya kuwasilishwa jambo lolote kutoka kwenye Mabaraza ya Pamoja. Jambo lolote linalotaka hatua za Serikali kuchukuliwa linapaswa kuwasilishwa na Baraza kwa Waziri ifikapo tarehe 15 Desemba. KUJAZA NAFASI WAZI Pale inapotokea nafasi ya mjumbe ipo wazi kwa sababu yoyote ile, nafasi yake itajazwa kwa utaratibu utakaoelezwa na Waziri na atakaa madarakani kwa kipindi kilichobakia. UTARATIBU WA KUTOA USHAURI NA UTATUZI WA MIGOGORO Pale ambapo Baraza Kuu la Pamoja la Utumishi wa Umma linapoamua kuishauri Serikali linapaswa kuwasilisha kwa Waziri ripoti ya maandishi iliyotiwa sahihi na Mwenyekiti au mjumbe mwingine aliyependekezwa kutia sahihi kwa niaba ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti au mjumbe mwingine aliyependekezwa kutia sahihi kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti. Waziri akishapokea ripoti hiyo ataipitia na kuishauri Serikali ipasavyo. Baraza litafahamishwa uamuzi wa Serikali katika kikao cha baraza kinachofuata. 65 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Makubaliano Makubaliano yoyote yatakayofikiwa na Baraza la Pamoja la Utumishi wa Umma kuhusu mgogoro utokanao na masharti na matakwa ya ajira ya watumishi wa Umma, yatakuwa kwa maandishi na kutiwa sahihi na Mwenyekiti au mjumbe yeyote aliyeteuliwa kutia sahihi kwa niaba ya Mwenyekiti na kupelekwa kwa Waziri. Waziri anapaswa kuyakubali makubaliano aliyoyapokea. Pale ambapo makubaliano hayo yatakubaliwa bila marekebisho yanakuwa TUZO Pale ambapo Waziri amefikiri ipo haja ya jambo hilo kutazamwa zaidi, atayarejesha makubaliano hayo kwenye Baraza kwa majadiliano zaidi. TUZO yoyote itakayotolewa itakuwa ya mwisho na itaibana Serikali na watumishi wa Umma ambao wanahusika na makubaliano hayo kwa kipindi cha miezi kumi na mbili kuanzia tarehe ambayo TUZO hiyo imetolewa. Hairuhusiwi kuleta kama ajenda ya majadiliano jambo lolote ambalo limo ndani ya makubaliano au kubadilisha makubaliano kabla ya kupata ruhusa ya Waziri isipokuwa pale ambapo muda wa miezi kumi na mbili umemalizika. TUZO iliyotolewa inapaswa kutangazwa na Waziri katika Gazeti la Serikali. BARAZA LINAPOSHINDWA KUFIKIA MAKUBALIANO Inapotokea Baraza kushindwa kufikia makubaliano katika mgogoro wowote, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watapeleka ripoti kwa Waziri, ripoti ambayo watakuwa wametia sahihi zao au imetiwa sahihi na walioteuliwa kufanya hivyo kwa niaba yao. Ripoti inayopelekwa kwa Waziri inapaswa ndani yake iwe na:(a) Muhtasari wa majadiliano ya Baraza na; (b) Taarifa ya jambo lililokuwa likijadiliwa. 66 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania UWASILISHAJI MGOGORO MAHAKAMANI Waziri akipokea ripoti ya Baraza anaweza kufanya yafuatayo:(a) Kurejesha mgogoro huo kwenye Baraza kwa Majadiliano zaidi iwapo atabaini:(i) Baraza halikuzingatia mambo ya msingi au yale yanayohusiana na mgogoro au; (ii) Baraza limezingatia mambo ambayo siyo ya msingi au ambayo hayahusiani na mgogoro. (iii) Baraza kulipa uzito usiokuwa na sababu suala au jambo husika. (iv) Baraza halikutumia taarifa muhimu zinazohusiana na mgogoro, kiasi cha kuhitaji juhudi zaidi zifanyike kutatua mgogoro kwa njia ya majadiliano. (b) Kuwasilisha mgogoro Mahakama ya Kazi. Mahakama ya Kazi inatakiwa kuwasilisha ripoti kwa Waziri baada ya kuupitia kwa makini mgogoro husika. Waziri anapaswa kurejesha mgogoro kwenye Baraza au kuuwasilisha Mahakama ya Kazi ndani ya siku ishirini na moja, hata hivyo iwapo Waziri katika mazingira maalum yanayolazimisha kuahirishwa kwa uwasilishaji au urejeshaji wa mgogoro anaweza kuahirisha kwa kipindi kisichozidi siku thelathini. UTOAJI WA TUZO Waziri anatakiwa awasilishe kwa Rais ndani ya siku kumi na nane ripoti aliyopokea toka Mahakama ya Kazi akiambatanisha maoni yake. Mara baada ya kupokea ripoti ya Mahakama na maoni ya Waziri Rais anaweza kutoa TUZO ya mgogoro. TUZO inayotolewa na Rais inaweza kuanza kutumika kinyume nyume kama itakavyoamuliwa na inapaswa itolewe ndani ya siku ishirini na moja kuanzia tarehe ripoti ya Mahakama ya Kazi na maoni ya Waziri yamewasilishwa kwake. 67 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Pale ambapo kwa maoni ya Rais yapo mazingira maalum yanayoweza kusababisha kuahirishwa kwa utoaji TUZO, utoaji TUZO utaahirishwa kwa kipindi atakachotaja Rais. KUCHAPISHWA KWA TUZO KATIKA GAZETI LA SERIKALI TUZO iliyotolewa na Rais ni lazima ichapishwe katika gazeti la Serikali na itaanza kutumika kuanzia tarehe ya kuchapishwa kwake. Iwapo itaelezwa kuwa TUZO itaanza kutumika kinyumenyume, TUZO itaanza kutumika tarehe iliyoonyeshwa kwenye TUZO. Kila TUZO itolewayo na Rais itaibana Serikali na watumishi wa umma wanaohusika kwa kipindi cha miezi kumi na mbili(12). Hairuhusiwi kuleta kama ajenda ya majadiliano jambo lolote ambalo limo ndani ya TUZO au kuleta maombi ya kubadilisha TUZO kabla ya kipindi cha miezi 12 kumalizika; isipokuwa kama itapatikana kabla ruhusa ya Waziri ya maandishi. MGOMO NA KUFUNGIA NJE Kila mtumishi wa Umma ana haki ya kushiriki katika mgomo au kufungia nje. Mtumishi wa Umma atashiriki katika mgomo au kufungia nje iwapo masharti yafuatayo yatakuwa yametimizwa:(a) Pawepo na mgogoro unaoendelea au lalamiko; na (b) Mgogoro au lalamiko halijatatuliwa; (c) Kura za kuunga mkono mgomo zimepigwa kwa usimamizi wa Afisa wa Kazi na watumishi walio wengi wameunga mkono mgomo; (d) Notisi ya siku 60 imetolewa kwa Serikali kuanzia siku kura ya kuunga mkono mgomo ilipopigwa. Mtumishi yeyote wa Umma atakayeshiriki katika mgomo au kufungia nje bila kufuata utaratibu atakabiliwa na hatua za kinidhamu. Watumishi wa Umma ambao kazi zao zikisimama au kuingiliwa kwa namna yoyote zitahatarisha maisha, afya au usalama wa watu, hawaruhusiwi kugoma au kufungia nje. 68 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania UCHOCHEZI Ni marufuku mtu ye yote yule awe mtumishi wa Umma au asiye mtumishi wa Umma, kushawishi au kuchochea mtumishi wa Umma kushiriki katika mgomo au kufungia nje kinyume cha sheria. Mtu wa namna hiyo:(a) iwapo ni mtumishi wa Umma atakabiliwa na hatua za kinidhamu. (b) Iwapo si mtumishi wa Umma atakabiliwa na hatua za kijinai. Endapo matokeo ya mgomo huo usiofuata sheria ni uharibifu wa mali za Muajiri, mtumishi ye yote wa umma aliyeshiriki katika mgomo au kufungia nje au mtu yeyote aliyechochea atapaswa kufidia uharibifu huo. KIZUIZI CHA UBAGUZI Mwajiri ye yote anakatazwa kumbagua mtumishi wa umma kwa sababu ya ushiriki wa mtumishi huyo katika mgomo au kufungia nje au kwa sababu ya kuwa kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi kilichoitisha mgomo huo. BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI MUUNDO WA BARAZA Baraza linaundwa na wajumbe thelathini na tatu kama ifuatavyo:(a) Mwenyekiti ambaye ni Katibu Mkuu anayehusika na watumishi wa Umma. (b) Makamu Mwenyekiti ambaye atachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe wanaowakilisha Vyama vya Wafanyakazi. (c) Watendaji saba wanaowakilisha Mkoa ambao watateuliwa kwa kuzingatia uwakilishi wa kanda kama ifuatavyo:(i) Kanda ya Kaskazini- Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. 69 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania (ii) Kanda ya Mashariki- Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. (iii) Kanda ya Kusini- Lindi Mtwara na Ruvuma (iv) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini- Iringa, Mbeya na Rukwa. (v) Kanda ya Magharibi- Kigoma, Tabora na Shinyanga. (vi) Kanda ya Ziwa- Mwanza, Kagera na Mara. (vii) Kanda ya Kati- Dodoma na Singida. (d) Watendaji tisa wanaowakilisha Wizara, Idara za Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:(i) Mjumbe mmoja anayeteuliwa na Waziri. (ii) Wajumbe watatu wanaoteuliwa na Katibu Mkuu Kiongozi. (iii) Kamishna wa Kazi. (iv) Afisa Elimu Mkuu. (v) Mjumbe mmoja kutoka ofisi ya Utumishi wa Umma, kitengo cha jinsia. (vi) Wajumbe watatu wanaoteuliwa na Waziri anayehusika na Serikali za Mitaa. (e) Wajumbe ishirini na moja kutoka miongoni mwa watumishi wa umma wataochaguliwa kama ifuatavyo:(i) Wajumbe saba wanaowakilisha watumishi wa Umma mikoani. (ii) Wajumbe saba wanaowakilisha Wizara na Idara za Serikali. (iii) Wajumbe saba wanaoteuliwa na Vyama vya Wafanyakazi. MUDA WA KUKAA MADARAKANI Wajumbe wa Baraza ukiacha Katibu Mkuu utumishi wa umma, Kamishna wa Kazi na Afisa Elimu Mkuu watakaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu tangu wateuliwe au kuchaguliwa na wanaweza kuteuliwa au kuchaguliwa tena. 70 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Mjumbe wa Baraza atakoma kuwa mjumbe iwapo:(a) Muda wa kukaa madarakani umekwisha. (b) Amekoma kuwa mtumishi wa umma. (c) Amehamishwa katika Mkoa wa Kanda nyingine. (d) Ameshindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo vya Baraza. Kwa wajumbe ambao ujumbe wao umetokana na madaraka yao ujumbe wao utakaoma mara anapoondoka katika madaraka hayo. KATIBU WA BARAZA Katibu na Katibu Msaidizi wa Baraza la Pamoja la Watumishi wa Umma watakuwa ndio Katibu na Katibu Msaidizi wa Baraza Kuu la Wafanyakazi. KUJAZA NAFASI WAZI Nafasi wazi itajazwa na mjumbe atakayeteuliwa au kuchaguliwa kwa kipindi kilichobakia. AKIDI Akidi ya Baraza ni wajumbe kumi na nane, uamuzi wa Baraza utafikiwa kwa wajumbe walio wengi kuunga mkono hoja hiyo. VIKAO Kikao cha Baraza kitafanyika mara moja kwa mwaka, kwa wakati na mahali itakapoamuliwa. Mwenyekiti anaweza kuitisha kikao kisicho cha kawaida iwapo itakuwepo haja ya kufanya hivyo. Vikao vitaongozwa na Mwenyekiti na asipokuwepo Makamu Mwenyekiti, wasipokuwepo wote, wajumbe watachagua Mwenyekiti wa muda miongoni mwao kuongoza kikao. 71 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania Kamati za Baraza G Baraza linaweza kuunda kamati mbali mbali kuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. G Kamati zinaweza kumshirikisha kama mjumbe wake mtu ye yote ambaye sio mjumbe wa Baraza kwa ajili ya kutoa utaalam katika baadhi ya mambo. Baraza lina uwezo wa kutengeneza Kanuni zake za kuendesha vikao vyake. Kazi za baraza Baraza lina kazi zifuatazo:(a) Kuishauri Serikali kuhusu taratibu za upandishaji vyeo na hatua za nidhamu kwa watumishi wa Umma. (b) Kuishauri Serikali kuhusu hatua za kuchukua kuhakikisha matokeo mazuri katika utoaji huduma. (c) Kuishauri Serikali kuhusu mabadiliko ya taratibu kuu za Serikali na masharti ya kazi na huduma. Baraza linapaswa kuwasilisha ripoti kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye akipokea ripoti hiyo anapaswa kuyapitia mapendekezo yake na kuyaasili kwa madhumuni ya kuboresha utumishi wa Umma. 72 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 73 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 74 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 75 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 76 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 77 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 78 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 79 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 80 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 81 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 82 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 83 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 84 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 85 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 86 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 87 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 88 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 89 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 90 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 91 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 92 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 93 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 94 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 95 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 96 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 97 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 98 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 99 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 100 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 101 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 102 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 103 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 104 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 105 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 106 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 107 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 108 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 109 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 110 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 111 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 112 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 113 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 114 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 115 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 116 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 117 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 118 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 119 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 120 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 121 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 122 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 123 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 124 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 125 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 126 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 127 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 128 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 129 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 130 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 131 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 132 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 133 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 134 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 135 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 136 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 137 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 138 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 139 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 140 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 141 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 142 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 143 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 144 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 145 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 146 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 147 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 148 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 149 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 150 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 151 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 152 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 153 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 154 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 155 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 156 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 157 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 158 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 159 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 160 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 161 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 162 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 163 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 164 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 165 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 166 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 167 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 168 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 169 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 170 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 171 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 172 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 173 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 174 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 175 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 176 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 177 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 178 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 179 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 180 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 181 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 182 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 183 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 184 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 185 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 186 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 187 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 188 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 189 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 190 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 191 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 192 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 193 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 194 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 195 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 196 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 197 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 198 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 199 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 200 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 201 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 202 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 203 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 204 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 205 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 206 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 207 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 208 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 209 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 210 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 211 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 212 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 213 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 214 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 215 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 216 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 217 Tafsiri Nyepesi ya Sheria za Kazi-Tanzania 218