Kiongozi cha Sheria Rehani, Upangaji na Ukodishaji Masuala yote haya yanafuata taratibu sawa kama ilivyoelezwa hapo awali chini ya Sheria ya Ardhi, Sura ya 113 kama sheria zilivyorekebishwa mwaka 2002 na marekebisho ya sheria hizi ya mwaka 2004 na 2005. Makosa ya Jinai yaliyoainishwa katika Sheria za Ardhi 1999 Sheria zote mbili zimeeleza kuwa ni kosa la jinai kwa mtu yeyote, kutoa habari za uongo kimaandishi au kwa mdomo kuhusiana na ugawaji wa ardhi au shughuli yoyote inayohusu ardhi au jambo lolote linalohusiana na sheria hizi za ardhi. Iwapo itabainika kuwa mtu ametenda kosa lolote la aina hii, atahukumiwa kifungo kisichozidi miaka mitatu, au faini isiyozidi shilingi milioni moja au vyote viwili, faini na kifungo kwa pamoja. USULUHISHI NA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI Ugawaji, umilikaji wa ardhi na maamuzi yanayofanyika kuhusiana na ardhi hayakosi migogoro na migongano ya hapa na pale. Ili kuhakikisha kuwa haki inatendeka na watu wote wanapata haki sawa katika kupata na kumiliki ardhi, migogoro hiyo inabidi itatuliwe kisheria. Hivyo basi Sheria hizi zote za ardhi zimeweka vyombo mbalimbali ili kushughulikia usuluhishi na utatuzi wa mingogoro hiyo. Vyombo hivi ni:• Baraza la Ardhi la kijiji • Baraza la Kata • Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya • Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi • Mahakama ya Rufani 20
Druckschrift
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
verfügbare Breiten