Kiongozi cha Sheria UTANGULIZI Ndoa ni taasisi ya zamani sana katika jamii. Ni kitu kilichoanza tangu mwanadamu alipoanza kuishi. Kwa kuwa ndoa ndio chimbuko la jamii yoyote ile, kila jamii ina utaratibu wa kufuata ili ndoa iwepo na jinsi ya kudumisha mahusiano yanayotokana na ndoa hiyo. Kabla ya ujio wa wageni, Watanganyika walikuwa wakiongozwa na taratibu za kimila katika masuala ya ndoa. Kila kabila au jamii walikuwa na utaratibu wao. Kuja kwa wageni hapa Tanzania kuliandamana na taratibu ngeni kuhusu mambo yanayohusu ndoa. Waarabu walipokuja walikuja na sheria na taratibu zao ambazo zilienda pamoja na imani ya dini ya Kiislam. Lakini kwa upande wa ndoa sheria zao hazijaingilia sana taratibu za kimila kuhusu ndoa. Wajerumani na hata Waingereza walikuja na mfumo wao. Mfumo huu ulienda pamoja na imani ya dini ya Ukristo waliyoileta iliyomtaka mwanaume awe na mke mmoja tu. Hii ilikuwa ni kinyume na utaratibu au mfumo wa kimila ambapo mtu aliweza kuoa wake wengi kadiri ya uwezo wake. Pia katika imani ya Kiislamu waumini wake waliagizwa kuoa wake si zaidi ya wanne kwa wakati mmoja. Kadhalika imani hizi za Ukristo na Uislamu zilikataza mtu kuoa au kuolewa na mtu wa dini tofauti. Ilipofika mwaka 1921 serikali ya kikoloni ilitunga sheria iliyozipa mahakama walizozianzisha mamlaka ya kushughulikia masuala ya ndoa. Mahakama zilizoanzishwa zilikuwa za aina mbili, yaani mahakama za kimila na mahakama za serikali kuu ya kikoloni. Mashauri yaliyohusu ndoa zilizofungwa kimila yalipelekwa katika mahakama za Kimila. Mahakama hizi zilikuwa zinawahudumia wale wenye asili ya Kiafrika tu. Kama ndoa ilikuwa imefungwa 26
Druckschrift
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
verfügbare Breiten