Druckschrift 
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
 

Kiongozi cha Sheria Sheria ya Kiserikali hutumika kwa Watanzania walioacha mila na desturi pamoja na watu wengine ambao si wazawa. Kumbuka Kama kuna wosia, mali hurithiwa kwa kuzingatia maelekezo ya wosia. Mgawo wa urithi katika Sheria ya Kiserikali Iwapo marehemu ameacha watoto; 1/3 ya mali hurithiwa na mjane/wajane, 2/3 hugawiwa sawa sawa kwa watoto wote. Kama hakuna watoto mali hugawiwa ifuatavyo; ½ hupata mjane/mgane ½ hupata wazazi wa marehemu au ndugu wa marehemu iwapo wazazi hawapo Ni muhimu kuelewa kwamba; Sio rahisi kuihakikishia Mahakama kuwa marehemu aliacha mila na desturi za kabila lake, hasa kama aliishi vijijini. Hivyo mara nyingi zaidi Sheria ya Kimila hutumika kugawa mirathi ya marehemu mzawa. Kesi za Mirathi zifunguliwe wapi? Ni vizuri sana kuelewa suala hili. Kesi zinazohusu kugawa mali ya marehemu kwa Sheria za Kimila, na ya Kiislam, lazima zifunguliwe Mahakama za Mwanzo na sio Mahakama nyingine zozote. Mahakama za Wilaya/Hakimu Mkazi na Mahakama Kuu hushughulikia tu mirathi ya marehemu pale ambapo Sheria ya Kiserikali hutumika.(Angalia: Sheria ya Mahakama za Mahakimu, Sura ya 11 ( Kama sheria zilivyorekebishwa mwaka 2002) kifungu cha 18(1) na 63(ii). 87