Druckschrift 
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
 

Kiongozi cha Sheria kikristo mahakama za kienyeji hazikuwa na mamlaka ya kusikiliza ndoa hiyo. Shauri kama hilo lilikuwa linapelekwa katika mahakama za serikali. Mahakama za serikali pia zilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri lolote toka kwa mtu yeyote. Zilipewa uwezo wa kutafsiri na kutumia sheria za mila ikiwa waliona sheria za mila hazipingani na utamaduni na sheria zao. Mwaka 1963 serikali iliondoa mfumo wa mahakama za kikoloni na kuleta muundo mpya. Pamoja na mabadiliko hayo sheria za mila kuhusu ndoa ziliendelea kutumika pamoja na mafundisho ya dini kuhusu ndoa. Mwaka huo huo wa 1963 serikali ilitangaza Sheria ya Hali za Watu. Sheria hii ilijaribu kukusanya taratibu mbali mbali za mila toka karibu makabila yote ya Tanganyika na kuziweka katika Tangazo la Serikali na. 279 la mwaka 1963. Pamoja na mkusanyo huu wa sheria za mila, mfumo mpya wa mahakama uliendelea kutumia taratibu karibu zile zile za Kiingereza(kikoloni). Kwa mfano, pale ambapo sheria fulani ya mila ilionekana kwenda kinyume au inapingana na mwelekeo wa serikali, sheria hiyo ilibatilishwa. Pamoja na msimamo huu wa serikali wa kupitisha mfumo mpya wa mahakama, dini zote ziliendelea kuhimiza waumini wao kufuata dini zao zinavyosema kuhusu ndoa. Tofauti na utatanishi ulijitokeza miongoni mwa waumini wa dini hizo ambao ulisababisha serikali kutunga Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971. Sheria hii ndiyo itakayojadiliwa kwa undani katika Sura hii. SEHEMU YA KWANZA Maana ya Ndoa Ndoa ni muungano wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao. 27