Kiongozi cha Sheria (j) Mashahidi wa ndoa Ili ndoa itambulike kisheria ni lazima ishuhudiwe na mashahidi wasiopungua wawili ambao wanaruhusiwa kisheria yaani umri wao usipungue miaka 18 na wafahamu kinachosemwa na kutendeka wakati wa kufunga ndoa. (k) Kuwa katika Eda Eda ni kipindi cha kukaa ndani kinachotolewa kwa mwanamke wa Kiislamu aliyeachika katika ndoa au aliyefiwa na mumewe, ili taratibu fulani za kidini zifanyike. SEHEMU YA PILI Aina za ufungaji wa Ndoa na Taratibu za Kufuata Kabla ya kufunga ndoa utaratibu ufuatao lazima uzingatiwe: (a) Kutoa Taarifa ya nia ya kuoana Kwanza kama mwanamke na mwanamume wanataka kufunga ndoa ni wajibu taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe kwa mfungishaji ndoa siku 21 kabla ya siku ya kufunga ndoa. Taarifa hiyo ioneshe mambo yafuatayo:Kama mwanamke ambaye ndoa ilifungwa Kiislamu anaolewa kipindi cha Eda hakijaisha basi ndoa hiyo ni batili. Kama atabadili dini baada ya kufiwa au kupewa talaka masharti ya Eda hayatambana. (i) Majina kamili na umri wa hao wanaotaka kuoana. (ii) Uthibitisho kwamba hakuna kipingamizi dhidi ya hiyo ndoa wanayotarajia kufunga. (iii) Majina kamili ya wazazi wao na sehemu wanakoishi. 31
Druckschrift
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
verfügbare Breiten