Kiongozi cha Sheria (iv) Hadhi ya wafunga ndoa. Yaani kama ni mwanamke ifahamike kama hajaolewa, ametalikiwa au ni mjane na mwanamume pia anapaswa kuwa hajaoa, au ana mke/wake wengine(hii ni kwa ndoa za kiserikali na Kiislamu) au kama ametaliki. (v) Kama muolewaji ana umri chini ya miaka 18, jina la mtu aliyetoa idhini ya yeye kuolewa kama yupo lionyeshwe. (vi) Kama ni ndoa ya Kiserikali au Kiislamu hapana budi kueleza kama ndoa ni ya wake wengi au inatazamiwa kuwa ya wake wengi na majina ya wake waliopo yatajwe. Pia katika fungu hili kama mtu anataka ndoa iwe ya mke mmoja anapaswa kueleza. (b) Kutangaza nia ya kufunga Ndoa Baada ya taarifa yenye maelezo haya kufikishwa kwa mfungishaji ndoa, yeye atawajibika kuitangaza nia hii ya kufunga ndoa. Sababu ya kufanya hivyo ni ili kama kuna mwenye kipingamizi na ndoa hiyo atoe taarifa. Matangazo haya hutolewa kulingana na aina ya ufungishaji wa ndoa. Kama ndoa inatarajiwa kufungwa kidini, matangazo hutolewa sehemu za ibada. Kama ni ndoa ya Kiserikali tangazo litabandikwa nje ya ofisi ya Msajili wa Ndoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya. Vipingamizi vya ndoa viko vya aina mbili, cha kwanza ni kile cha kisheria yaani kama ndoa itakayofungwa itakuwa batili. Kipingamizi cha pili ni kama muoaji ana mke au wake wengine tayari, hivyo mke au wake wanaweza kutoa kipingamizi kama uwezo wa muoaji kifedha ni mdogo kiasi 32
Druckschrift
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
verfügbare Breiten