Druckschrift 
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
 

Kiongozi cha Sheria Msajili wa Ndoa. Ndoa itafungwa katika Ofisi ya Msajili au mahali pengine popote palipotajwa katika leseni yake ya kufungisha ndoa. (c) Ndoa ya Kimila Ndoa inaweza kufungwa kimila iwapo mmoja wa wafunga ndoa au wote wawili wanafuata sheria za mila za kabila fulani. Mdhamini wa ndoa za kimila ni Katibu Tarafa. Ndoa ya kimila hufungishwa na mtu anayetambulika kimila kuwa ana uwezo huo. Ni muhimu sana Katibu Tarafa kuhudhuria kwenye ufungishaji huo wa ndoa kwani ndiye atakayehusika na kuleta vyeti vya ndoa kutoka kwa Msajili. Ufungaji Ndoa nje ya Nchi Waziri wa Sheria ana mamlaka ya kuteua baadhi ya maofisa ubalozi kuwa wasajili wa ndoa. Ni lazima msajili aridhike kuwa masharti yote yametimizwa ndipo afungishe ndoa. Kuna masharti ya nyongeza kama angalau mmoja wa wafunga ndoa hawa ni Mtanzania. Pia kama mmoja wa wafunga ndoa si Mtanzania ni lazima Msajili aridhike kuwa ndoa inayokusudiwa kufungwa itatambulika kisheria katika nchi ambayo huyo mmoja wa wafunga ndoa ni mkazi. Utaratibu unaotumika kufungisha ndoa hizi ni sawa na ule unaotumika katika kufungisha ndoa za Kiserikali. Dhana ya Kuchukulia Ndoa Kuna dhana inayokanushika kuwa mwanamume na mwanamke wakiishi pamoja huweza kuchukuliwa kuwa ni mke na mume mbele ya sheria japokuwa hawakuwahi kufunga ndoa. Ili dhana hii iwepo ni lazima yafuatayo yathibitishwe. (1) Lazima ithibitike kwamba mwanamke na mwanamume wameishi pamoja kwa muda wa miaka 2 au zaidi kwa mfululizo. 34