Druckschrift 
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
 

Kiongozi cha Sheria kumtunza mke na watoto kuna wakati inawezekana mume akasafiri kwa muda mrefu na hakuacha fedha au alizoacha zimekwisha, au mume amemtoroka mke na kumwachia watoto. Mke ana haki ya kukopa fedha kwa jina la mumewe au kuweka rehani mali ya mumewe. Mke ana uwezo wa kutumia mali ya mumewe ambayo inahamishika au kutumia fedha za mumewe zilizoko mikononi mwake kwa ajili ya kununulia mahitaji ya muhimu kwa ajili yake na watoto wake ni halali kisheria. Haki hizi zinakuwepo kama mke na mume wanaishi pamoja au kama wametengana kwa mapatano kuwa mume atatoa matunzo na mume amepuuzia mapatano hayo. Jambo la kuzingatia kwa makini hapa ni kuwa ili haki ya kutumia mali ya mume iweze kuwapo ni lazima mahitaji yanayonunuliwa yawe ni yale ambayo kama mume mwenyewe angekuwepo, angekuwa kuyanunua lake. na uwezo kulingana na wa pato Haki ya kuishi katika nyumba ya ndoa Nyumba ya ndoa ni nyumba ambayo mume na mke wanaishi wakati wa ndoa. Hata kama wana nyumba nyingi ni nyumba moja tu ndiyo inayochukuliwa kama nyumba ya ndoa. Pamoja na kuwa nyumba ya ndoa inaweza kuwa mali binafsi ya mke au mume, nyumba hiyo haiwezi kuuzwa, kuwekwa rehani au kuchukuliwa na mtu mwingine kama zawadi bila ya makubaliano ya wote wawili. Ikiwa mume atafanya chochote kwenye nyumba hii bila ya makubaliano na mke, mke atakuwa na haki ya kuishi katika nyumba hiyo hadi hapo Mahakama itakapotoa maamuzi ya kuvunja ndoa hiyo, kutengana au amri ya matunzo. Kadhalika mume naye anayo haki hiyo hiyo iwapo mke ndiye mwenye 40