Kiongozi cha Sheria Wosia wa Maandishi Kwa mwosia anayejua kusoma na kuandika ni vema wosia wake ukawa katika maandishi. Wosia huu unatakiwa uandikwe kwa kalamu ya wino au kalamu isiyofutika au upigwe chapa. Tarehe ya wosia ni muhimu hivyo iandikwe. Katika wosia wanahitajika mashahidi wawili. Mwandishi wa wosia(mwosia) aweke saini katika wosia. Kama mwosia hajui kusoma na kuandika aweke alama ya kidole gumba cha mkono wa kulia. Mashahidi washudie saini au alama ya mwosia na wenyewe waweke saini zao kwenye wosia. Mwosia atataja mtu au watu ambao anapenda wasimamie ugawaji wa mali baada ya kifo chake.(Msimamizi/Wasimamizi wa mirathi). Mambo ya kuzingatia Mwenye kuacha wosia anategemewa kuwapa urithi warithi wake wa halali na wengine mwenyewe. anaowapenda 1. Mwosia anaweza kumnyima urithi, mrithi halali iwapo tu mrithi, amemkosea mambo mazito kama: (a) Mrithi amezini na mke wa mwosia. (b) Mrithi amejaribu kumuua, kumshambulia au kumdhuru vibaya mwosia(au kumtendea mama wa mwosia mambo haya yaliyotajwa). (c) Mrithi bila sababu ya msingi, hakumtunza mwosia wakati wa shida, njaa au maradhi. 2. Mtu anaweza kumrithisha rafiki yake vitu au mali zake alizokuwa akizitumia mwenyewe au sehemu ya 93
Druckschrift
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
verfügbare Breiten