Kiongozi cha Sheria mali yake. Lakini fungu la rafiki lisizidi la kila mrithi halisi. Wosia katika Sheria za Kiserikali Hakuna tofauti kubwa na wosia katika Sheria za Kimila bali wosia huu unatarajiwa uwe katika maandishi. Hivyo vipengele vyote vya wosia wa maandishi vinatumika. Mwosia anaweza kufuta au kuongeza maneno mengine kwa kuandika maandishi mengine ambayo itabidi yazingatie masharti ya uandikaji wa wosia. Wosia katika Sheria ya Kiislamu Kwa mujibu wa Sheria ya Kiislamu, mwosia haruhusiwi kuusia mali yake yote. Huruhusiwa kuusia 1/3 tu ya mali yake. Sehemu 2/3 ni lazima ifuate taratibu za kiislamu za ugawaji mali ya urithi. Mahali pa kuhifadhi wosia Wosia unaweza kuhifadhiwa sehemu yoyote yenye usalama kuepusha uwezekano wa kufanyiwa mabadiliko na mtu asiye mwosia. Hivyo, wosia waweza kutunzwa mahakamani, msikitini, kanisani, kwa mwanasheria n.k. Kwa hali yoyote ile, ni muhimu mtu mzima aliyefanikiwa kuwa na mali kuandika wosia. Umefika wakati wa kuondokana na fikra potofu kuwa, mtu akiandika wosia anajichuria kufa. Vifo vipo na sasa hivi hali ni mbaya sana kwani watu wengi wanakufa kwa ajali, magonjwa kama shinikizo la damu, UKIMWI, uti wa mgongo na kadhalika. Tabia ya kuandika wosia ni muhimu kwa mtu anayejali familia yake ambayo anaweza kuacha wosia unaotambulika kisheria. 94
Druckschrift
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
verfügbare Breiten