Druckschrift 
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
 

Kiongozi cha Sheria (2) Lazima ithibitike kuwa umma unaowazunguka unawachukulia na kuwapa heshima kama mke na mume. (3) Lazima ithibitishwe kuwa watu hao walikuwa na uwezo wa kuwa mke na mume wakati walipoanza kuishi pamoja na kama walikuwa na umri uliokubalika kisheria. hii wana haki na wajibu sawa kama ilivyo katika ndoa nyingine zisizo na kasoro. Kadhalika watoto waliozaliwa katika ndoa ya namna hii ni halali na wana haki zote kisheria. Ni vitu gani vinafanya Ndoa kuwa Batilifu? Sababu zinazoweza kufanya ndoa kuwa batilifu ni: (4) Ni lazima pia ithibitishwe kuwa kati ya hao wawili au wote hakuna aliye na ndoa inayoendelea. SEHEMU YA TATU Ndoa Batilifu na Sababu zinazoweza kuifanya Ndoa kuwa Batilifu Ndoa batilifu ni ndoa ambayo itachukuliwa kisheria kuwa ni ndoa halali hadi hapo amri ya kuivunja itakapotolewa. Ndoa batilifu ni halali kama ndoa nyingine isipokuwa ina kasoro fulani. Wanandoa katika ndoa 1. Maradhi ya zinaa Kama wakati wa kufunga ndoa mmoja wa wafunga ndoa alikuwa na maradhi ya zinaa na yule asiye na ugonjwa kama wakati wa kufunga ndoa alikuwa hajui lolote kuhusu maradhi hayo anaweza kulalamika mahakamani na ndoa ikavunjwa. 2. Kukataa kwa makusudi kuitimiliza ndoa Kama baada ya kufunga ndoa mmoja wa wana ndoa atakataa kutimiliza ndoa kwa makusudi anayekataliwa ana haki ya 35