Kiongozi cha Sheria • Kama kuna mmojawapo ana ndoa inayoendelea ambapo anazuiwa kuingia katika ndoa nyingine mfano mwenye ndoa ya kikristu, muislamu ambaye tayari ana wake wanne au mwenye ndoa ya kiserikali/kiislamu ambaye wakati wa kufunga ndoa alisema ni ndoa ya mke mmoja. • Iwapo mahakama au baraza la usuluhishi umekataza ndoa isifungwe lakini ndoa ikafungwa. • Kama wote au mmoja wao hakuingia kwenye ndoa bila hiari. • Kama wanandoa wote hawakuwapo kwenye tukio la kufunga harusi. • Kama wanandoa kwa kufahamu kuwa mfungishaji hana mamlaka lakini wakamwacha afungishe ndoa. • Iwapo ufungishaji ndoa haukushuhudiwa na mashahidi. • Kama ndoa inalenga kuwa ya muda. • Iwapo mwanamke yuko katika eda. Kugeuza Ndoa Watu waliooana wana uhuru wa kugeuza ndoa yao pale wanapofuata taratibu zilizowekwa kisheria. Kabla ya kufanya uamuzi wa kugeuza ndoa ni budi wanandoa wakubaliane kuhusu uamuzi huo. Kitendo cha kugeuza ndoa hufanywa mbele ya Hakimu wa Wilaya au Jaji ambapo wanandoa watatoa tamko la maandishi lenye saini zao na Hakimu au Jaji aliyeshuhudia naye huweka saini yake. Katika kugeuza ndoa, ndoa ya kiserikali, ya kimila au ya Kiislamu inaweza kugeuzwa kuwa ya mke mmoja kama kabla ya kugeuza ilikuwa ni ndoa ya wake wengi. Ikumbukwe kuwa kubadilisha dini pekee hakubadilishi hadhi ya ndoa. Vile vile ndoa ya kikristo haiwezi kugeuzwa kuwa 38
Druckschrift
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
verfügbare Breiten