Druckschrift 
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
 

Kiongozi cha Sheria UTANGULIZI SEHEMU YA KWANZA Maana ya Talaka S heria inayosimamia masuala ya talaka ni sheria ya Ndoa ya 1971. Na kwa mujibu wa sheria hiyo, Talaka ni ruhusa ya kisheria ambayo mume au mke hupewa wakati anapomwacha mwenzie. Chombo chenye mamlaka ya kutoa talaka Chombo pekee chenye uwezo wa kuvunja ndoa ni mahakama. Kwa kawaida mahakama hutoa talaka kwa ndoa ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi. Lakini mahakama inaweza kutoa talaka hata kama ndoa haijadumu kwa kipindi hicho cha miaka miwili iwapo mlalamikaji atatoa sababu nzito sana za kuthibitisha kuwa anapata mateso makubwa. Kutengana Kutengana sio talaka. Kutengana maana yake ni mume na mke kuishi mbalimbali. Kutengana kunaweza kuwa kwa mapatano kati ya mume na mke bila ya kufika mahakamani. Aidha kutengana kunaweza kutokana na amri ya mahakama kuwatenganisha wanandoa ikiwa mmoja wao atakuwa amepeleka ombi hili mahakamani. Kutengana kwa mapatano Mume na mke kwa hiari yao wanaweza kukubaliana watengane ikiwa wameona hawaelewani katika maisha yao. Mapatano haya inashauriwa yawe ya maandishi. Mambo ya kuzingatia kwenye mapatano ni:­i. Mume na mke wote wameridhia kuishi mbalimbali. ii. Kutokubughudhiana, yaani hakuna ambaye atakwenda 45