Druckschrift 
Kiongozi cha sheria : na kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake
Entstehung
Einzelbild herunterladen
 

Kiongozi cha Sheria kuwa na hofu ya kuamini kwamba hapo baadaye ataumizwa mwili au afya yake. Kulawiti Kulawiti maana yake ni kumwingilia mtu kinyume na maumbile. Kichaa Ili talaka iweze kutolewa ni lazima madaktari wawili bingwa wa magonjwa ya akili wathibitishe kuwa ugonjwa huo hautapona. Vipigo katika ndoa ni sehemu ya ukatili; hakuna mwanandoa anayeruhusiwa kumpiga mwenzake. Kuzembea wajibu kwa makusudi Mume ana wajibu wa kumtunza mkewe, kwa kumpa chakula, mahali pa kulala na mavazi yanayofaa kulingana na hali yao ya maisha. Mke pia ana wajibu wa kumtunza mume ikiwa mke huyo anao uwezo na mume hawezi kujipatia pato lolote,kwa sababu ya maradhi au maumivu ya mwili. Hivyo basi kama mume anaishi na mke, lakini hampi matumizi hata kidogo, au anatoa matumizi kidogo sana kwa mkewe ukilinganisha na uwezo wake na hali yao ya maisha, 47